Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Rachid Talbi El Alami katika ofisi za Bunge hilo zilizopo Jijini Rabat nchini Morocco leo tarehe 18 Septemba, 2023.

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mabunge ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya kilimo, viwanda na biashara.

Aidha, Dkt. Tulia ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Serikali ya Morocco kwa vifo vya watu zaidi ya 3000 na madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mapema mwezi huu.

Pia amepongeza juhudi zilinazofanywa na Mfalme wa Mohammed wa vi wa Morocco katika kukabiliana na maafa pamoja na changamoto zilizotokana na tetemeko hilo.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto), amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Rachid Talbi El Alami katika ofisi za Bunge hilo zilizopo Jijini Rabat nchini Morocco leo tarehe 18 Septemba, 2023.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto), akiwa ameambatana na mwenyeji wake Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Rachid Talbi El Alami akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake katika nchi hiyo katika ofisi za Bunge hilo zilizopo Jijini Rabat nchini Morocco leo tarehe 18 Septemba, 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...