Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari( MAELEZO) Gerson Msigwa ameelezea kuwa kupitia Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika(AGRF) Tanzania itaieleza kwa kina fursa zilizopo katika sekta ya kilimo ikiwemo ardhi ya kutosha inayofaa kwa kilimo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msigwa amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini ni jambo kubwa na kutumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa na dhamira njema ya kukuza uchumi sambamba na kuinua maisha ya Watanzania.

Akielezea kuhusu sekta ya kilimo Msigwa amesema Serikali kwa kutumia mkutano huo inayaeleza mataifa mengine ya Afrika kuwa Tanzania kuna ardhi zaidi ya ekari milioni 44 inayofaa kwa kilimo.

Amefafanua chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Tanzania imeamua kuwekeza kwenye kilimo hivyo ametoa rai mataifa mengine ya Afrika kuja kuwekeza katika sekta hiyo kwa kushirikiana na Watanzania kuzalisha mazao chakula na biashara.

Msigwa ameeleza yapo mazao kama mbegu za mafuta ,mchele, ngano, ,mahindi pamoja na ufugaji huku akisisitiza mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika ni muhimu kwa watanzania.

Ameongeza mkutano huo unafanyika wakati Serikali ya Awamu ya Sita ikiwa imeweka mipango na mikakati ya kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo.

Akifafanua zaidi kuhusu mkutano huo amesem mataifa 70 yameshiriki na kufanya kuwa na wageni zaidi ya 4000 na wageni hao wanatumia fedha ambazo zinaingia kwenye mikono ya Watanzania.

"Tunampongeza Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayofanya na matokeo yake yanaonekana.Kufanyika kwa mkutano huu umefanya kuwepo kwa fursa nyingi lakini hata unaposikiliza mijadala utasikia mifano mingi inayotolewa inahusu Tanzania."

Pamoja na hayo, Msigwa ametoa rai kwa waandishi wa habari kushiriki na kuripoti mkutano huo ili umma wa Watanzania ufahamu kinachoendelea.

"Uandishi wa habari ni sanaa hivyo lazima waandishi wa habari wakati mwingine tujue watu wanataka nini na wakati gani, tumekuwa na kasumba kutoa taarifa ambazo wakati mwingine zina mitazamo fulani , ni vema waandishi wakajenga utamaduni kuripoti habaro ambazo wananchi wanazitaka."

Amesisitiza vyombo vya habari vinaumuhimu mkubwa katika mkutano huo na kutoa mwito kwa taasisi zinazoshiriki jukwaa hilo kutumia vyombo hivyo kueleza shughuli wanazofanya wananchi wafahamu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...