Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo, imetanabaisha kuwa Dkt. Ndumbaro alifungiwa miaka saba na uongozi wa TFF uliopita, hata hivyo Dkt. Ndumbaro hakukubaliana na uamuzi huo na alikata rufaa kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya Shirikisho hilo kupinga adhabu hiyo.
“Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF chini ya uongozi wa sasa ilisikiliza rufani hiyo mwaka 2017 ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro alishinda, hivyo kuondolewa adhabu ya kufungiwa,” imeeleza taarifa hiyo ya TFF.
Hata hivyo, taarifa hiyo imetaarifu umma kuwa kwa sasa Waziri Dkt. Damas Ndumbaro ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...