Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Ali Mwinyi akizungumza leo Septemba 07, 2023 katika mkutano wa pembeni katika jukwaa la mifumo ya chakula Afrika  linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akizungumza leo Septemba 07, 2023 katika mkutano wa pembeni katika jukwaa la mifumo ya chakula Afrika  linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Matukio Mbalimbali  leo Septemba 07, 2023 katika mkutano wa pembeni katika jukwaa la mifumo ya chakula Afrika  linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Ali Mwinyi leo Septemba 07, 2023 ameendesha halambee ya washirika mbalimbali kuchangia utekelezaji wa mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT).

Halambee hiyo imefanyika katika mkutano wa pembeni wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika (AGRF) unaoendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaa, ukiwa na

Akizungumza wakati wa halambee hiyo Raid Dkt. Mwinyi amesema kuwa kumekuwa na utashi wa kisiasa unaokua kwa kasi barani Afrika hususani Tanzania unaolenga kuwawezesha vijana na wanawake katika kilimo biashara.

Amesema, utashi huo unaonekana kufuatia juhudi mbalimbali ikiwemo kupitishwa mikataba ya tamko la mpango wa utekelezaji wa vijana, kunzishwa kwa dawati la vijana katika mpango mpya wa ushirikiano wa pamoja na uwezeshaji mpango wa BBT.

Rais Dkt. Mwinyi amesema, serikali imeandaa mikakati shirikishi na kutekeleza mipango ya kusaidia vijana na wanawake katika sekta ya kilimo biashara katika hatua za uwezeshaji wa mradi wa BBT utaongeza ajira kupitia mfumo wa chakula.

Amesema kutokana na kukua kwa mifumo ya kidigitali inayosimamia mabadiliko ya uchumi wa dunia kumekuwa na ongezeko la kasi kwa vijana kuwa sehemu ya ukuaji wa uchumi Afrika kupitia kilimo.

“Bado kuna changamoto ya ushiriki mdogo wa vijana na wanawake katika sekta za kilimo na uvuvi kutokana na upatikanaji mdogo wa rasilimali za uzalishaji, ujuzi na ukosefu wa mitaji.” Amesema Rais Dkt. Mwinyi

Akizungumza kuhusiana na vijana amesema vijana wana hamu ya kuwekeza sehemu zenye matokeo ya haraka.

Rais Dk. Mwinyi amesema ili kufikia mafanikio yapo maeneo yanahitaji ufumbuzi ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii vijijini ili kupunguza wimbi la vijana ambao wanao uwezo wa kushiriki katika kilimo kuhamia mjini.

“Pia ni mujimu kumaliza tatizo la kukosekana kwa masoko, vikwazo vya kimazingira na mabadilioo ya tabia nchi, kukosekana kwa miundombinu ya uzalishaji na kutafuta ufumbuzi katika uwekezaji wa teknolojia.” Amesema

Akizungumzia uwezeshaji wa vijana na wanawake katika sekta ya kilimo amesema ufunguo wa milango ya ajira ni kilimo ambacho kinaweza kuwa chanzo cha kupunguza umaskini na matokeo ya uzalishaji wa chakula na kujiongezea la thamani.

Ili kufikia malengo ya vijana na wanawake Rais Dkt. Mwinyi amesema serikali ya Tanzania imejidhatiti katika kuwawezesha vijana na wanawake kufikia malengo yao, ikiwemo kuwepo kwa mazingira wezeshi katika kilimo biashara.

Kwa Upande wa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, lengo la serikali ni kukusanya zaidi ya dola bilioni 2 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BBT unaoisha mwaka 2030.

Amesema, hatua hiyo itawezesha ukuaji wa uchumi kwa kuwa kilimo kinachangia asilimi 25 ya Pato la Taifa huku asilimia 70 ya Watanzania wanategemea kilimo, kinatoa  asilimia 75 ya ajira na kuchangia mauzo ya nje ya nchi kwa asilimia 85.

Mradi wa BBT unalengo la kujumuisha vijana zaidi ya milioni 16 katika mfumo rasmi wa kiuchumi kupitia kilimo biashara kwa kuwapa elimu na uwezeshaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...