katika nia ya kuhamasisha weledi zaidi katika sekta ya masoko nchini Tanzania, Chama cha wataalamu wa Masoko Tanzania (TMSA) kinatarajiwa kufungua kongamano la masoko kwa mara ya nne na kutoa tuzo za masoko kwa mara ya tatu mfululizo katika vipengele 20 tofauti kwa mwaka huu.
Tuzo hizi za masoko 2023 zitafanyika tarehe 27 Oktoba jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Blue Saphire pembezoni mwa hoteli ya Ramada.
Tukio hili litafunguliwa na kongamano saa tatu asubuhi, na majira ya saa kumi na mbili jioni ugawaji wa tuzo hizo zitafanyika.Tangu mwaka wa 2021, TMSA imetumia tuzo hizo ili kuakisi juhudi na mafanikio ya watu binafsi, mashirika, na wasomi ambao wanaleta mabadiliko katika nyanja ya masoko.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa TMSA, Dkt. Emmanuel Chao (PhD), alieleza jinsi masoko kuwa nguzo muhimu ili kuhakikisha ukuaji wa kampuni na kuleta faida.
Alisema, "Katika biashara yoyote, idara ya masoko ni ya kipekee, kwani inajumuisha kati ya asilimia 30 na 40 ya bajeti ya biashara, na ndio kati ya msingi wa kudumisha biashara yoyote".
Aliendelea, ‘kwahiyo, kama TMSA, tutatumia fursa hii kuhimiza makampuni na watendaji kuwa na weledi zaidi katika hii idara. Na kwa bahati nzuri, katika TMSA, tayari tunatoa programu za masoko.
Pia tuko kwenye mazungumzo na Taasisi ya Chartered Marketing Institute ya nchini Uingereza UK kushirikiana kwenye uandaaji wa programu mbalimbali za masoko. Nia yetu ni kuhakikisha soko la ndani linafaidika zaidi kwa kuzalisha wataalamu waliohitimu na wenye uelewa zaidi wa soko la Afrika kuliko soko la nje’’.
‘Aidha, tungependa kuwashukuru wadhamini wetu ambao wametoa usaidizi muhimu katika kufanikisha tukio hili. Hizi ni: Smart Codes, Hessa Africa, Imperial Marketing and Communication, Bremex Marketing and Communication, Integrated Marketing Communication, Kango, 360, Attwood Marketing and Communication na nyinginezo’.
Mmoja wa wadhamini wakuu kutoka kampuni ya SmartCodes, Iche Omari ambae aliiwakilisha kampuni hio alisema kuwa tuzo hizo zitakuwa chachu katika kuchochea ukuaji wa sekta ya masoko.
Alinukuliwa, "Tuko pamoja na TMSA katika utoaji wa tuzo za TMSA, na tuna matumaini yetu ni kuwa huu ni mwelekeo sahihi wa kuhamasisha ubunifu na weledi miongoni mwa wafanyabiashara wa Tanzania’.
Mchakato wa kuchagua na kuteua washindi wa tuzo uliendeshwa mtandaoni kupitia tovuti ya www.tma.tmsa.or.tz/nomination, ambapo watu binafsi na mashirika yaliteuliwa. Baada ya mchakato wa uteuzi huo, timu ya majaji wenye uzoefu ilipitia uteuzi uliopendekezwa na washindi waliochaguliwa.
Mkurugenzi wa Chama cha wataalamu wa Masoko Tanzania, Dkt. Emmanuel Chao (PhD) (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza tuzo za masoko na kongamano la 2023 litakalofanyika tarehe 27 Oktoba kwenye ukumbi wa Blue Saphire jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni mwakilishi na mdhamini kutoka kampuni ya Bramex Sylvia Joseph, wa kwanza kulia ni Gloria Malikita kutoka kampuni ya Smartcodes (mdhamini) na wa pili kushoto ni Iche Omari kutoka Smartcodes (mdhamini).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...