Na Rahma Khamisi Maelezo   13/9/2023

 

Uongozi wa Skuli ya Trifonia umesema utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwajali na kuwathamini wazee wasiojiweza nchini.

 

Aakizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa Vitu mbalimbali kwa wazee katika Kituo cha Kulelea Wazee Welezo, Mkurugenzi wa Skuli hiyo Grace Bernad amesema  hatua hiyo itasaidia kuwafanya wazee hao kujiona wapo sawa na watu wengine.

 

Alisema msaada huo  utawafajiri wazee hao   na kuwasaidia  katika mahitaji yao ya kila siku .

 

Aidha alieleza kuwa wamefaraijika kuona wazee wanaotunzwa katika nyumba hizo na  Serikali ya Mapinduziaya Zanzibar  kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee  zinaendelea vizuri na kuahidi kusaidia wazee hao mara kwa mara .

 

Hata hivyo wamewashauri wadau ,na taasisi zenye uwezo kuwapitia na kuwafariji wazee hao  kwa kupatia Misaada mbalimbali ya kujikimu katika mahitaji yao

 

"Tumetoa msaada huu  kwa lengo la kuwafanya wazee hawa kuona kuwa bado tunawajali na kuthamini nguvu zao kabla ya  uzee kwani na wao walikuwa kama sisi ",alisisitiza.

 

Nae Mkuu wa Kituo cha kulelea  Wazee wasiojiweza Welezo Khamisi Ali Haji amesema kuwa hatua iliyo chukuliwa na Skuli hiyo ni njema kwani wameisaidia Serikali katika kutimiza majukumu yao.

 

Hata hivyo walishukuru na kupongeza ujio wa Skuli hiyo katika kituo hicho na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo.

 

Katika Msaada huo Wazee hao walipokea vitu mbalimbali ikiwemo dawa ,unga ,sukari ,mafuta na mashuka kutoka kwa Uongozi wa Skuli ya Trifonia ikiwa ni mrejesho kwa jamii  kuelekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

 

Mkurugenzi wa Skuli ya Trifonia Grace Peter Myamba akikabidhi vitu mbalimbali kwa Wazee wa Kituo cha kulelea Wazee Welezo kushoto ni Afisa Wazee Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee Zanzibar Pili Sadala Mussa
Mwakilishi wa Kamati ya Wazee Skuli ya Trifonia  Dorice Mwakasendo akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa  wazee wanaoishi nyumba za kutunzia Wazee Welezo ikiwa ni mrejesho wa Skuli hiyo kwa jamii kuelekea kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

 

Picha  na Rahma Khamis Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...