NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WAKUU wa Vyombo vya Habari vya Umma, Wadau wa TEHAMA na Wanahabari zaidi ya 200 kutoka nchi 14 wanachama Kusini mwa Afrika , Afrika Mashariki na Magharibi wanatarajia kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.

Mkutano huo wa 30 wa mwaka wa SABA na Mkutano wa 7  unazungumzia masuala ya TEHAMA katika kukuza teknolojia ya Habari na Utangazaji Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba amesema mkutano huo utajadili kwa kina nafasi ya TEHAMA na mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa kidijiti Afrika ili kuleta maendeleo endelevu na kuonyesha maboresho makubwa yaliyofanyika hivi karibuni katika teknolojia ya Habari.

"Lengo lingine ni kujadiliana habari, kupanua uelewa wa masuala ya TEHAMA na kupeana mbinu mbalimbali za kuboresha teknolojia ya habari na utangazaji ili kuendana na mabadiliko kiteknolojia ya sasa". Amesema

Aidha amesema kuwa Mkutano huo utafanyika katika hoteli ya Golden Tulip ambapo mgeni rasmi ambaye atafungua anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Umoja na Mashariki ya Utangzaji ya Umma Kusini mwa Afrika (SABA).

Pamoja na hayo amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa utachangia ongezeko la pato la Taifa linalotokana na Utalii.

"Tumeichagua Zanzibar kwa kuwa ni mojawapo ya maeneo muhimu ya utalii katika nchi yetu. Wageni hawa watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Zanzibar na kujionea uzuri na upekee wa eneo hili la nchi yetu". Amesema

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka SABA utakaofanyika katika Wilaya ya Mjini Magharibi, Zanzibar Oktoba 10-12,2023. 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...