Njombe

Watu 6 ambao ni raia wa kigeni waliokuwa wakisafiri kwa njia haramu wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika kijiji cha Iyai kata ya Luduga Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe barabara kuu ya Makambako kuelekea mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe John Makuri Imori amesema ajali hiyo imetokea mapema alfajiri ya kuamkia leo,huku watu wengine nane wakiwa majeruhi na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya wanging'ombe huku Polisi wakiendelea kumsaka Dereva na kondakta wa gari aina ya Scania yenye namba za usajili T.501 AGJ waliosababisha ajali hiyo iliyokuwa pia na Raia wa kigeni ambao wanasadikika kuwa ni kutoka ethiopia.
 
"Aajali hii ilihusisha gari namba T 501 AGJ aina ya Scania iliyokuwa na tela lake lenye namba T595 ANJ iliyokuwa inatoka Makambako kuelekea Zambia baada ya kufika hapa tumekuta ndani ya gari kuna mizigo mingi sana ya vifaa vya ujenzi lakini pia baada ya kufungua tela tumekuta watu ambao ni raia wa kigeni na bahati mbaya hatujapata hati zao zozote za kuwatambulisha"amesema Kmanda Makuri

Kamanda Makuri amesema kuwa gari inamilikiwa na moja ya kampuni kutoka Arusha na sasa wanaendelea kufuatilia zaidi raia hao wanatokea nchi gani ambapo taarifa zaidi zitatolewa ambapo ametoa wito kwa wananchi kuacha mara moja biashara hiyo ya kusafirisha raia wa kigeni bila utaratibu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...