Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufungua Maadhimisho ya 20 ya Wahandisi yanayotarajia kuanza Septemba 13 hadi 15 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe, amesema Waziri Mkuu Majaliwa anatarajia kufungua rasmi maadhimisho hayo Septemba 14, 2023 huku akieleza ni fursa kwao kwa ajili ya kuongeza wigo katika kufikia malengo

Ameongeza katika maadhimisho hayo zaidi ya Wahandisi 4,000 kutoka ndani ya nje ya nchi wanatarajia kushiriki na kupata fursa ya kuonesha kazi zao na kujadili mada mbalimbali za kitaalamu zenye lengo la kuleta tija kwa Taifa.

"Katika katika maadhimisho ya wiki ya wahandisi watapokea mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa."

Amefafanua Wahandisi watapata fursa ya kujadili pamoja na viongozi wa Wizara na Taifa katika kutoa muongozo hasa nini wanapaswa kufanya ili waendelee kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

“Pia tutawatambulisha wahandisi wapya pamoja na kula kiapo kwa ajili ya kufanya kazi kwa uzalendo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa na sio yao binafsi pamoja na kushiriki zoezi la kuchangia damu salama, ” amesema Mhandisi Kavishe.

Amesema wakati umefika wa kuwandaa watu wao kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika miradi mikubwa ambayo inatekelezwa hapa nchini.

Mhandisi Kavishe amesema washiriki watapata fursa ya kushiriki mada mbalimbali za kitaaluma ambazo zimelenga ushiriki katika ujenzi wa Taifa pamoja na ushirikishwaji wa rasilimali za ndani (Local Content) na kuzingatia uweledi na kasi ya mabadiliko (Skill Menegment).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Mhandisi Benedict Mukama, amesema kuwa mpaka sasa maandalizi yamekamilika, huku akieleza kuwa Wahandisi wataonesha teknolojia za ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mhandisi Mukama amesema kuwa Wahandisi wengine kutoka mataifa mbalimbali Duniani watashiriki kwa njia ya mtandao.

“Viongozi wengi wa Kitaifa watashiriki wakiwamo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, wabunge, huu ni mkutano pekee unaofanywa na Wahandisi mara moja kwa mwaka” amesema Mhandisi Mukama.

Amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa Wahandisi kwa sababu unawaweka pamoja kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kufika malengo tarajiwa.

Tangu mwaka 2003 Wahandisi wamekuwa na utamaduni wa kuwa na Wiki ya Wahandisi kwa ajili kuonesha kazi pamoja na kujadili mada zenye lengo la ujenzi wa Taifa.
Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Wahandisi yanayotarajia kuanza Septemba 13,2023 katika Ukumbi wa Mlimani City.(kushoto)Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Mhandisi Benedict.(na kulia)Msajili Msaidizi Uendelezaji wa Taaluma Mhandisi Veronica Ninaluro.
(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV)Mkutano ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...