Ecobank Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Shule Direct wametoa msaada kuwalipia walimu kujifunza masomo kupitia mfumo wa Shule Direct, kutoa msaada wa vishikwambi13 kwa matumizi ya Wanafunzi pamoja na kutoa pesa kwa ajili ya ukarabati chumba cha Maabara ya Kompyuta  ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii katika maadhimisho ya uwajibikaji wa kijamii kwa kila mwaka ambayo huzishirikisha jamii zote ndani ya bara la Afrika.

 Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu amesema benki hiyo inautaratibu wa kila mwaka wa kurudisha kwa jamii ambapo leo wameamua kutoa msaada wa vishikwambi13 kwa matumizi ya Wanafunzi pamoja na kutoa pesa kwa ajili ya ukarabati chumba cha Maabara ya Kompyuta  katika shule ya Sehondari ya Mugabe iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam

Amesema Ecobank Tanzania inadhamini mchango mkubwa wa shule ya Sekondari ya Mugabe kwa kuzalisha wataalam mbalimbali hapa nchini hivyo kutoa msaada huo itakuwa chachu kuweza kuinua kiwango cha ufahulu katika shule hiyo.

Naye Mkuu wa shule  Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome ameishukuru Ecobank Tanzania kwa kuweza kutoa msaada katika shule hiyo kwani kufanya hivyo inawapa nguvu ya kuendelea kutoa Huduma kwa jamii.

Siku ya Ecobank ni tukio la kila mwaka ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka 2013, likiwa na mlengo wa kufanyika kila mwaka ikibeba kaulimbiu maalumu. Kaulimbiu hizi zimekuwa zikitoa Elimu kwa Vijana Wadogo Afrika (2013); Kuzuia na Kudhibiti Malaria (2014); kila mtoto wa Kiafrika ana haki ya kuwa na maisha bora ya baadaye (2015); Elimu ya TEHAMA shuleni na kuboeresha Afya ya Uzazi (2016); Usimamizi wa maji salama (2017); Makazi ya yatima (2018); Saratani (2019); Ugonjwa wa kisukari (2020) , Afya ya Akili(2021) na msaada wa vyereheni, khanga pamoja na Taulo za Kike katika Hospitali ya CCBRT (2022)
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu (kushoto) akikabidi vishikwambi Mkuu wa shule  Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome (kulia) vitakavyotumika kujifunzia  masomo kupitia mfumo wa Shule Direct ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii ambapo Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akizungumza wakati wa kukabidhi vishikwambi katika shule ya  Sekondari ya Mugabe kwa ajili ya kujifunzia  masomo kupitia mfumo wa Shule Direct ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii.
Mkuu wa shule  Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa benki ya Ecobank Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu mara baada ya kukabidi Vishikwambi, kuwalipia walimu kujifunza masomo kupitia mfumo wa Shule Direct pamoja na kukarabati chumba cha Maabara ya Kompyuta katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania  wakishuhudia ugawaji wa vishikwambi katika shule ya Sekondari ya Mugabe
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu  akizungumza na uongozi wa shule ukiongozwa na Mkuu wa shule  Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome kuhusu na mba benki hiyo ilivyojipanga kukarabati chumba cha Maabara ya Kompyuta katika shule hiyo  ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii hasa kurudisha kwa jamii inayoizunguka.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akiwaogoza wafanyakazi wa Ecobank Tanzania kupaka rangi ikiwa ni kufaya ukarabati wa chumba cha Maabara ya Kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Mugabe iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii ambapo Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania Furaha Samalu akiendelea kupaka rangi kwenye chumba cha Maabara ya Kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Mugabe iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu wakiwa kweye picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mugabe wakiongozwa na Mkuu wa shule hiyo Mathew Mchome  pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
 Mkuu wa shule  Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome akiwakaribisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa msaada ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii katika maadhimisho ya uwajibikaji wa kijamii kwa kila mwaka ambayo huzishirikisha jamii zote ndani ya bara la Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...