Na.Khadija Seif,Michuziblog

MABONDIA wajiweka tayari kuelekea pambano la 'Usiku wa Moto',  huku bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Mgender 'Ibrahim Class' amesema lazima mpinzani wake apigwe katika ardhi ya nyumbani Oktoba 28,2023 katika Ukumbi wa PTA 77  Jijini Dar es Salaam.

Ibrahim atashuka ulingoni kucheza na Xion Tau Su kutoka China katika pambano la raundi 10 uzito wa kati .

Akizungumza Wanahabari Leo Oktoba 25,2023 Jijini Dar es Salaam Bondia  Ibrahim Class amesema amemaliza mazoezi sasa anasubiri siku ya pambano ifike. ambapo pamba

" Nimejiandaa vizuri kupambana na mpinzani wangu kwa sababu nilikaa kambi Tanga chini ya kocha wangu Master Habibu Kinyogoli."

Promota wa pambano hilo, Hamisi Kombucha amesema baada ya kumaliza pambano hilo wanatarajia kuandaa mapambano mengine katika ukanda wa nchi zilizo Sadc.

"Kwa mara kwanza Tanzania kunachezeka mkanda wa Ubingwa wa WBC Afrika, kupitia bondia, Fadhili Majiha ambaye atacheza na Bongani Mahlangu kutoka Afrika Kusini."

Pia ameeleza kuwa kutakuwa na mapambano tisa siku hiyo huku hali ya usalama imekaa vizuri kutokana na mazingira na ulinzi ulioimarishwa.

Kwa upande wake Bondia Fadhili Majiha amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia anavyompiga mpinzani wake, Bongani Mahlangu kutoka Afrika Kusini.

Majiha ameongeza kuwa  amejipanga kuhakikisha anampiga Mahlangu raundi zote 12 na kubakisha mkanda nyumbani.

"Nimejipanga kucheza ndani ya kiwango, Mahlangu mara nyingi anakuja nchini kupigana na mabondia wa kawaida, awamu hii amekutana na kisiki."

Majiha anashuka ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kumpiga Renz Rosia kutoka Ufilipino kushinda mkanda wa UBO.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...