Na Janeth Raphael- MichuziTv Dodoma

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeitaka Wizara ya maji kutafuta mradi wa muda mfupi ili kuhakikisha wananchi wanapata maji kabla ya kukamilika kwa mradi wa kutoka ziwa Victoria ambao unatarajiwa kuwa suluhisho la upungufu wa maji katika jiji la Dodoma na vitongoji vyake.

Ameyasema hayo leo Oktoba 27,2023 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maji naazingira Jackson Kiswaga katika ziara ya kamati hiyo walipokagua utekelezaji wa mradi wa visima unaogharimu kiasi cha bilioni 4.8 ambapo wameridhishwa na Ujenzi wake.

Kiswaga ametoa maelekezo Kwa Wizara ya Maji na DUWASA kuongeza Kasi ya utekelezaji wa Mradi huo ili kuhakikisha wananchi wanapata Maji Kwa wakati uliyokusudiwa.

Kamati hiyo, imepongeza juhudi za Serikali kwa kuchukua hatua na kutoa fedha ili kupunguza uhaba wa huduma ya maji katika jiji la Dodoma ambapo kuna upungufu wa lita milioni 65, lita milioni 68 ndio zinazozalishwa hivi sasa.

Hivi sasa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inachimba kisima kikubwa cha mita 300 ili kuongeza wingi wa maji kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo imepata Fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji ,unaofanyika katika eneo la Kolon jijini Dodoma.

Ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga amepongeza juhudi zilizofanyika katika ujenzi wa kituo hicho na kusisitiza kitumike kuwakusanya wataalamu mbalimbali wa rasilimali za maji kutoka kona zote za Dunia ili kuisaidia nchi katika uendelezaji wa rasilimali za maji.

Kwa upande wake ,Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amesema kituo hicho kitakapokamilika Pamoja na kazi nyingine, kitatumika katika masuala ya utafiti wa rasilimali za maji.

Amesema ujenzi wake umefika asilimia 75 na inatarajiwa kitakamilika mapema mwaka 2024 na eneo la ujenzi wa kituo hicho limetumika katika masuala ya utafiti wa maji chini ya ardhi kabla ya uhuru, tangu mwaka 1956.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema mradi wa maji wa Nzuguni utekelezaji wake umefika asilimia 93 na ndani ya saa 24 wananchi wataona mabadiliko ya huduma ya maji kupitia mradi huo.

Mradi huo wa Maji Nzuguni ukikamilika utakuwa unazalisha maji lita Milioni 7 Kwa siku na utahudumia Wananchi zaidi ya 75,000 katika Kata ya Nzuguni ,Ilazo ,Kisasa Nyumba 300 na maeneo mengine ya Jirani

 
 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...