SERIKALI kupitia wizara ya Afya  imesema itaendelea kuwajengea uwezo nje ya nchi  wataalamu wa Afya  ili  waweze kuongeza ujuzi wa namna bora ya  kutengeneza vifaa tiba  vitakavywahudumia wananchi kwa muda mrefu.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt.Grace Maghembe wakati akizungumza mkoani Iringa mara baada ya kufungua  na kukabidhi karakana ya  matengenezo  ya vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Karakana hiyo imejengwa  na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya  Uswis kupitia mradi wa  Health Promotion and  Systeam [HPSS ]  na kugharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 85.

Dkt.Grace alieleza kuwa lengo la serikali kuwapeleka wataalamu hao wapatao  zaidi ya 30   katika nchi ya Hungali na China  ni kuwaongezea ujuzi wa namna ya utengenezaji vifaa  viba  ili viweze kutoa huduma kwa muda mrefu

 Aliongeza kuwa Serikali imeamua kujenga karakana hizo kila Hospitali kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za Afya kunzia  Hospitali ya rufaa, wilaya na Vituo vya Afya nchi nzima.

Awali akitoa taarifa fupi ya ukarabati  na uwekaji wa vifaa tiba na samani  Meneja mradi wa [HPSS] Ally Kebby  alieleza kuwa zaidi ya milioni 85 zimetumika kukamilisha  ujenzi wa mradi huo  unaotajwa kuwa mwarobaini  wa  uhaba wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake mhandisi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Rainfrida Kadinda akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za karakana alisema kuwa kutokana na Serikali kuboresha  mazingira ya kazi  hivi sasa kutawezeshakufanya kazi kwa ufanisi zaidi ukilinganisha na hapo awali.


‘’Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajiliya ununuzi wa vifaa tiba na kuboresha huduma za afya hapa nchini’Alisema

 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...