Njombe
Patrick Mwinuka (35) mkazi wa mtaa wa Igangidung'u uliopo kata ya kivavi mjini Makambako wilayani Njombe,amekutwa amefariki baada ya kujinyonga kwa kamba kwenye nyumba ambayo amekuwa akiishi mjini humo huku bado sababu zikiwa hazijafahamika.
Mkuu wa upelelezi wilaya ya kipolisi Makambako Gotifrid Kimboy amewataka wananchi kushirikisha watu wao wakaribu pindi wanapopitia changamoto za kiafya ama uchumi badala ya kujinyonga.
Aidha Kimboy ameongeza kuwa matukio mengi ya kujinyonga,mauaji hata ukatili ambao unafanyika katika wilaya ya Kipolisi Makambako yanahusishwa na imani za kishirikina,wivu wa mapenzi,ulevi kupita kiasi pamoja na migogoro ya ardhi.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Igangidung'u Emmanuel Gadau amesema Patrick Mwinuka amejinyonga kwenye nyumba aliyopewa aishi baada ya kuajiliriwa na Jaliwa Mbwilo ili ahudumie mifugo na kufanya kazi za shamba huku balozi wa eneo hilo Regani Kabelege akibainisha kuwa Mwinuka alikuwa anasumbuliwa na mgongo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...