Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Wapigania Uhuru (Mashujaa) Lusaka Zambia tarehe 24 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati viongozi mbalimbali walipokuwa wakiweka Mashada ya maua kwenye eneo la Mnara wa Kumbukumbu ya Wapigania Uhuru (Mashujaa) wa nchi hiyo katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo Jijini Lusaka tarehe 24 Oktoba, 2023.

Matukio mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Taifa la Zambia katika mnara wa kumbukumbu ya Wapigania Uhuru wa Taifa la Zambia uliopo Mtaa wa Uhuru Jijini Lusaka. Zambia inaadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zambia Hayati Kenneth Kaunda (Presidential Burial site, Embassy Park Jijini Lusaka tarehe 24 Oktoba, 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...