Mwandishi wetu. Babati 

MICHUANO ya 16 ya Chemchem CUP 2023 ambayo inalenga kupiga vita ujangili wa Twiga imezinduliwa katika eneo la hifadhi ya jamii ya Burunge WMA wilayani Babati mkoa Manyara.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Babati.Lazaro Twange kwa niaba ya Mkuu wa mkoa, amesema michuano hiyo licha ya kuinua vipaji vya michezo lakini inaendeleza uhifadhi.

Twange amesema vijiji 10 ambavyo vinaunda Burunge WMA,vinapaswa kushirikiana na Taasisi ya chem chem ambayo imeweza shughuli za utalii na uhifadhi katika eneo hilo.

"Tunatarajia nyie muwe mabalozi wazuri wa uhifadhi ,mtowe taarifa za wanaojihusisha na ujangili lakini pia muendelee kunufaika na uhifadhi"alisema

Awali Mkurugenzi wa chemchem association Fabia Bausch alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa imejuwa na faida kubwa kushirikisha jamii katika uhifadhi kupitia uhifadhi.

Fabia alisema mwaka huu kwa mara ya kwanza kutakuwa na timu 10 za wasichana na za mchezo wa soka, timu 16 za wanaume na timu 7 za vijana.

Amesema taasisi hiyo imetenga kutimia zaidi ya sh 99.2 million kufanikisha michuano ya mwaka huu.

Awali Mwenyekiti wa michuano hiyo,Elasto Belela amesema maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika ambapo timu.zote shiriki tayari zimepewa seti za jezi na mipira kwa maandalizi.

Amesema mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya sh 2.5 milioniwa pili 1.5 milioni wa tatu 1 milioni .kwa upande wa wasichana mabingwa watapata 1.5 milioni,mahindi wa pili million Moja na mshindi wa tatu 500,000.

Kwa michezo kwa vijana chini ya miaka 18 mshindi atapata milioni Moja wa pili 600,000 na WA tatu 400,000.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...