Kampuni ya Bia ya Serengeti imetangaza kundi lingine la wanafunzi wanaofadhiliwa kupitia programu yao ya Kilimo Viwanda, inayolenga kutoa fursa ya elimu kwa wanafunzi wasio na uwezo wanaosoma kozi za kilimo.
Katika miaka minne iliyopita, Programu ya Kilimo Viwanda imesaidia zaidi ya wanafunzi 300 katika harakati zao za kusomea kozi ya kilimo, huku ikijenga mfumo endelevu wa wataalamu wenye ujuzi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kilimo nchini Tanzania.
Akizungumza katika tafrija ya kutoa ufadhili wa masomo, Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries, Obinna Anyalebechi alisema, “Ufadhili huu ni sehemu ya ahadi yetu ya kusaidia maendeleo ya kilimo nchini. Tunaamini kuwa program hii itasaidia sana kuimarisha rasilimali ya wataalamu wa kilimo nchini kwa kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji na hatimaye mapato”.
Mkurugenzi alisema kwamba mwaka huu, SBL itawasaidia wanafunzi wapya watano ambao watajiunga na wanafunzi tisa ambao tayari wanasomea taaluma za kilimo katika Shule ya St. Maria Goretti huko Iringa. Upanuzi huu wa program unaonyesha dhamira ya Serengeti Breweries ya kusaidia utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo, lengo kuu likiwa kuongeza uzalishaji na mapato ya wakulima.
Mkurugenzi wa Mnyororo wa Ugavi wa Serengeti Breweries, Bw. Alfred Balkagira pia alisifu, “Programu hii inachochea vipaji vya ndani, ikiongeza uwezo wa upatikanaji wa malighafi za ndani. Hatua hii sit u inapunguza gharama bali pia inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa jamii za wakulima zinazozunguka, ikijenga uhusiano thabiti kati ya SBL na jamii ya eneo hilo”.
Zaidi ya hayo, wanafunzi wanaosoma kupitia program hii huenda wakawa mabingwa wa mbinu endelevu za kilimo, na hivyo kuathiri kwa njia chanya mchakato wa upatikanaji na uzalishaji. Dhana zao mpya na mawazo ya ubunifu zitasaidia kuongeza ufanisi na kusawazisha upatikanaji wa malighafi za SBL kutoka kwa wakulima kwa ajili ya uzalishaji wa bia, kama shayiri, mahindi na mtama.




Mkurugenzi Masuala ya Umma wa SBL, John Wanyancha akizungumza katika hafla hio iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Maria Goretti, Iringa.


Mwananfunzi mpya wa programu hio, Annastazia Koko akizungumza katika hafla hio iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Maria Goretti, Iringa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...