Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto), akizungumza jambo na Balozi wa Tanzania nchini Uswisi Mhe. Hoyce Temu (katikati) pamoja na Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) katika ukumbi mdogo wa Mikutano wa Bunge la Angola Jijini Luanda wakati wa Mkutano wa 147 wa IPU unaoendelea nchini humo.

 

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Vyombo vya Habari nchini Angola leo tarehe 24 Oktoba, 2023 akijinadi na kueleza sababu za yeye kugombea nafasi hiyo. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewaeleza namna atakavyohakikisha anasimamia misingi ya Umoja huo kwa kuongeza Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akishiriki Mkutano wa 147 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Luanda nchini Angola leo tarehe 24 Oktoba, 2023. Katika Mkutano huo pamoja na mengineyo, unatarajiwa kufanyika Uchaguzi wa Rais mpya wa Umoja huo ambapo Dkt. Tulia ni miongoni mwa Wagombea waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 24 Oktoba, 2023 akizungumza katika mdahalo wa Wagombea Urais wa kiti cha IPU katika Jukwaa la Wabunge Wanawake kwenye IPU katika ukumbi mdogo wa Bunge la Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa IPU akiwaomba wampigie kura katika Uchaguzi wa Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...