Na Mwandishi wetu

KATIKA Kuadhimisha siku ya miji duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba 31, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa Tanzania ( TALGWU) kimesema kuwa haki za Wafanyakazi ni haki za binadamu

 Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo na Katibu wa Chama hicho, Rashid Mtima wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 31, 2023. Amesema ieleweke kwamba  haki za wafanyakazi ni sehemu ya muhimu ya ukuaji endelevu na jumuishi wa miji hapa nchini na duniani kote.

Amesema mafanikio yanayopatikana katika ukuaji wa miji unachagizwa na utendaji kazi bora wa wafanyakazi waliopo katika sekta mbalimbali wakiwa na jukumu la kuhakikisha eneo la kazi linakuwa salama bila manung'uniko na kulipa umuhimu suala la haki watendaji hao.

"TALGWU inatambua kazi inayofanyika katika miji hapa nchini hasa usimamizi wa miundombinu ya barabara, usafi wa mazingira, utunzaji wa taka ngumu na maji pamoja na shughuli zote za Maendeleo zinazo lenga kukuza miji hapa nchini zinazofanywa na watumishi wa Umma ambao ni wanachama wetu."

Amesem kuwa  TALGWU inatambua  jukumu hilo na wanahitaji wafanyakazi  wanafanya kazi katika mazingira bora ba salama huku wakipatiwa hazi za msingi ambazo zitawaongezea ari na morali ya kufanya kazi kwa ubora.

Awali Mtima amesema kuwa siku ya Miji duniani hutumika kama fursa ya kukuza nia ya Jumuiya ya Kimataifa katika ukuaji wa miji duniani, kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi katika kushughulikia  changamoto za ukuaji wa miji na kuchangia maendeleo endelevu ya miji duniani kote.

 Mtima ametoa wito kwa serikali kutambua umhimu wa miji na upangaji wa miji katika majiji yote yanayokua kwani miji ndio inauwezo wa kulisha miji yote na vijijini kwa sababu kunamwingiliano huduma za kijamii. tika miji na vijiji.

Pia amesema Changamoto zilizopo katika miji ndio fursa na serikali ikitaka kutoa huduma kwa wananchini lazima iweke kipaumbele katika miji na kutambua haki za wafanyakazi wa miji.


Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa Tanzania (TALGWU), Rashid Mtima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 31, 2023 wakati wa kutoa tamko la siku ya wafanyakazi wa TALGWU ambayo hufanyika kila mwaka 31, 2023 duniani kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...