Njombe
Tume ya ushindani (FCC) nyanda za juu kusini imesema kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha anadhibiti bidhaa bandia kwenye mazingira yake kuokoa madhara yoyote yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya bidhaa zisizo halisia.
Wito huo umetolewa na Dickson Mbanga mkuu wa ofisi ya tume ya ushindani nyanda za juu kusini wakati akizungumza na wananchi kwenye maonesho ya nne ya SIDO kitaifa yanayofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
"Juhudi ziendelee kufanyika katika kudhibiti bidhaa bandia na sasa hii sio kwa FCC peke yake hata wananchi wenyewe wanawajibu wa kuhakikisha wanakuwa ni wadau katika kudhibiti bidhaa bandia"amesema Mbanga
Vile vile ametoa wito kwa wajasiriamali kuelewa haki na wajibu wa mlaji wa bidhaa na wajibu wao katika bishara wanazozifanya ili kuhakikisha wanaleta bidhaa bora sokoni na kujiepusha na uagizaji wa bidhaa bandia zinazowazulu walaji nchini.
Vile vile ametoa wito kwa wajasiriamali kuelewa haki na wajibu wa mlaji wa bidhaa na wajibu wao katika bishara wanazozifanya ili kuhakikisha wanaleta bidhaa bora sokoni na kujiepusha na uagizaji wa bidhaa bandia zinazowazulu walaji nchini.
Diana Augustine ni afisa ulaghabishi kutoka tume ya ushindani amesema lengo kubwa la kufika kwenye maonesho ni kuwaeleimisha wananchi kujua maana ya bidhaa bandia.
"Bidhaa bandia ni yeyote inayokuwa imetengenezwa kwa kuiga nembe ya mzalishaji halisi bila ridhaa ya yule mwenye nembo na kuna tofauti kubwa kati ya bidhaa bandia na bidhaa hafifu"amesema Diana
Nao baadhi ya wajasiriamali akiwemo Hadija Said wanasema matumizi ya bidhaa bandia ni hatari sana kwa mlaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...