Na Jane Edward, Arusha ..

Wanachama wa vilabu vya waandishi wa habari kutoka Kilimanjaro, Manyara na Arusha wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kuelezea matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela katika mafunzo ya siku mbili yaliyo wakutanisha wataalamu kutoka ofisi ya Taifa ya  takwimu yanayofanyika kwa siku mbili jijini Arusha.

Mongela amesema kuwa waandishi wa habari ni sekta muhimu katika kutoa elimu kwa jamii juu ya namna sensa ilivyo fanyika vizuri na kwa uwazi na kuelezea matokeo ya sensa hiyo kwa upana wake.

"vyombo vyetu vya habari viandae mijadala inayohusu matokeo ya sensa ili kupanua upeo wa wananchi katika kuangalia maswala ya maendeleo kwa wananchi wetu "Alisema Mongela

Amesema kuwa Lengo la Serikali ni kuona matokeo ya
Sensa yanawafikia wadau wote hususani wananchi ili waweze kuyatumia
katika shughuli zao binafsi na pia kuzitumia katika kushiriki kikamilifu
katika maendeleo ya nchi ikiwemo kushiriki katika kupanga, kufuatilia na
kutathmini shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali .

 Aidha amesema kama ilivyokuwa kwa  wakati wa kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa, hivi sasa ni wakati wa kuyawasilisha kwa wananchi kwa lugha rahisi na kwa weledi kupitia taaluma ya habari.

Awali wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi Kamisaa wa sensa na spika mstaafu Anna Semamba Makinda amesema sensa ya mwaka huu imefanikiwa kwa asilimia 99.99 ambapo takwimu hizo za sensa zinakubalika na kuaminika Duniani.

Amesema mategemeo yake ni kuona waandishi wanafahamu masuala ya takwimu na kutumia lugha rahisi katika uandishi wao ili wananchi waweze kuelewa.

Amesema katika matumizi ya takwimu kwa waandishi wa habari itawasaidia katika taarifa zao mbalimbali kwa kuwa huwa hazidanganyi na kuwataka waandishi wasifanye kazi kwa hofu.


 Kamisaa wa sensa Anna Semamba Makinda akibadilishana mawazo na viongozi wa sensa kutoka Zanzibar katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...