Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

Oct 24

Watu watatu wamepoteza maisha katika ajali ya barabarani ikihusisha magari mawili kugongana uso kwa uso huko Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani majira ya saa 3 usiku Oktoba 23/2023.

Aidha watu wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Kluger lenye namba T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dsm likiwa na watu 7 wa familia moja  aligongana na gari lenye namba T.851 AQC aina ya Scania.

Lutumo alisema katika ajali hiyo watu wanne walijeruhiwa ambao ni Amina Kondo miaka 77 na mtoto wa mwaka mmoja Abdallah Ally wote wakati wa Manzese Dar esalaam.

Majeruhi wengine wawili bado hawajafahamika majina yao kutokana na kutoweza kuzungumza,, wote walikimbizwa Hospitali ya Msoga Chalinze kwa matibabu

Majeruhi hao wanne pamoja na  watu watatu waliopoteza maisha wote walikua kwenye gari hilo dogo la Kluger.

Miili ya marehemu imehifadhiwa kituo cha afya Lugoba  Chalinze.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...