Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua sherehe za miaka 20 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) na kupata fursa ya kutembelea banda la Maonyesho la Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) na kupata maelezo juu ya Kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kutoka kwa Mkuu wa Mafunzo Chuo cha CATC Bw. Didacus Mweya.
Chuo cha CATC kinatoa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi katika masual
a mbalimbali ya Usafiri wa Anga. Chuo cha CATC ni chuo kinachotambulika kitaifa na Kimataifa chenye ithibati ya TCAA , NACTVET na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). Na ni miongoni ya vyuo sita Afrika vinavyotambuliwa na ICAO vinavyoa kozi za usalama wa Usafiri wa Anga na miongoni mwa vyuo 35 duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...