NA
K-VIS BLOG, DODOMA
MKURUGENZI
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma, amewataka wafanyakazi wa Mfuko huo kudumisha
Ushirikiano ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama na wadau wa Mfuko
wakiwemo waajiri, wanufaika na wafanyakazi pale watakapopata ajali ama kuugua
kutokana na kazi.
Dkt.
Mduma ameyasema hayo Oktoba 4, 2023 kwenye ofisi za WCF, jijini Dodoma, wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya WCF ya wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja
iliyoanza Oktoba 2, 2023.
Maadhimisho
ya wiki ya Huduma kwa wateja ni tukio la kimataifa ambalo linaangazia umuhimu wa
huduma kwa wateja na watu wanaotoa huduma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano
kwa watoa huduma na wateja, ambapo mwaka huu wa 2023 imebeba kaulimbiu ya “Ushirikiano kwa Huduma Bora.”
“WCF
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tumekuwa tukifanya kazi na kutoa huduma kwa
ushirikiano kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema, kuanzia ngazi ya
mkurugenzi mkuu, Menejimenti mpaka kwa afisa wa kawaida.” Amesema na kuongeza.. Katika maisha yetu tunafurahia kufanya kazi
na kutoa huduma kwa pamoja tena kwa
ushirikiano mkubwa bila kujali yupi ni wa ngazi ipi.” Amesisitiza Mkurugenzi
Mkuu.
Amesema
kama ilivyo desturi ya wafanyakazi wa WCF, kwa kauli mbiu ya mwaka huu “TEAM
SERVICE” au HUDUMA KWA USHIRIKIANO, inakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa
kutambua ushirikiano ambao utawezesha kutoa huduma bora zaidi kwa wateja na
wadau bila kusubiri wale walio katika madawati ya mapokezi.
Katika ofisi za WCF za Dar es Salaam, Temeke, Ilala, Arusha, Mbeya, Mwanza, Geita na Morogoro, wakuu wa ofisi hizo wamewahimiza wafanyakazi wenzao kuhakikisha wanadumisha ushirikiano baina yao wenyewe lakini na wanaowahudumia ili kudumisha taswira nzuri iliyopo ya Mfuko huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...