Na.Ashura Mohamed -Monduli

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amemuagiza Meneja wa Miradi ya Maji Vijijini Mkoani Arusha(RUWASA) Mhandisi Joseph Makaidi pamoja na Mhandisi wa Maji wilaya hiyo Nevile Msaki kutoa kiasi Cha shilingi milioni 240 Kwa ajili ya Ukarabati wa bwawa katika kata ya Lepurko wilayani Monduli mkoani Arusha.

Akizungumza mara baada ya kutembelea bwawa hilo Waziri Aweso alisema kuwa zoezi la Ukarabati linatakiwa kuanza mara Moja siku ya Jumatatu (November 13) na kukamilika baada mwezi mmoja Ili kuwezesha wananchi kupata maji ya kutumia wakati Serikali ikiendelea na mchakato wa kuwapatia maji safi na salama wakazi wa wilaya hiyo kupitia mradi mkubwa uliosainiwa.

"Nataka niwaeleze kuwa kilio chenu serikali imekisikia na Ajenda ya Maji ni ya Kitaifa na haswa Ajenda ya kumtua mama ndio kichwani hivyo basi hapa hakuna tutakachowaamvia tukaelewana zaidi mnahutaji maji hivyo ninawataka RUWASA kuhakikisha kazi inaanza mara Moja ndani ya Mwezi mmoja bwawa likamilike na December nitakuja kuzindua"Alisema Aweso

Aidha Waziri Aweso amewatoa hofu wakazi wa kata ya Monduli na kuwahakikishia kuwa serikali itahakikisha kuwa mradi huo wa Maji wilayani Monduli unakamilika mara Moja.

Kwa kuwa mmeomba kwanza bwawa hili basi nataka niwahakikishie kuwa litakamilika na msimu huu wa mvua hizi litawasaidia lakini mradi ambao tunasaini utatatua changamoto ya maji kabisa hivyo muwe na Imani na serikali yenu"Alisisitiza Waziri

Katika hatua nyingine serikali imetia saini mkataba wa zaidi ya shilingi Bilioni 27 kwa ajili ya mradi wa maji katika vijiji 17 unaotarajiwa kutatua kero ya muda mrefu ya maji inayonawakabili wananchi wilayani humo.

Akizungumzia mradi huo meneja wa RUWASA mkoa wa Arusha mhandisi JOSEPH MAKAIDI amesema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka miwili huku wananchi nao wakielezea matumaini yao kutokana na mradi huo.

Hafla hiyo imefanyika katika kata ya Lepurko eneo la Nanja wilayani Monduli ikihusisha mkataba wa mradi wa maji toka jiji la Arusha wenye Thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 20 kwenda vijiji 13 na mkataba mradi wa maji kwenda vijiji vinne vya Makuyuni wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.

Viongozi mbalimbali wameshuhudia utiaji saini huo ukiongozwa na waziri wa maji Jumaa Aweso,mbunge wa jimbo hilo Fredrick Lowassa,Mkuu wa wilaya Joshua Nassary,mwenyekiti wa Halmashauri Isack Joseph.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso Akizungumza na wananchi eneo la nanja wilayani Monduli mkoani Arusha katika hafla ya Utiaji Saini Mradi wa Maji wa Zaidi  ya shilingi  bilioni 27.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...