Na Mwandishi Wetu
KATIKA jitihada za kuandaa wahitimu wanaoendana na soko la ajira duniani, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeanzisha ushirikiano na kampuni ya RSM Eastern Africa ili kuwajengea uwezo wanafunzi wake katika eneo la uhasibu na elimu ya fedha.
Kupitia ushirikiano huo RSM itatoa mafunzo kwa wanafunzi wa chuo hicho katika maeneo matatatu ambayo ni ukaguzi wa hesabu, za fedha, elimu ya kodi, elimu ya kutoa ushauri wa kitaalamu.
Akifungua mafunzo hayo jana chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Emmanuel Munishi, alisema mnbali na CBE, mafunzo hayo yatatolewa pia kwa wanafunzi wa vyuo vingine.
“CBE itakuwa ni kituo tu au Hub ya mafunzo hayo kwa taasisi zote za elimu ya juu Tanzania na kwenye program hii tunatarajia kuwanufaisha wanafunzi 3,000 wanaosomea Shahada za Uhasibu, uhasibu na fedha pamoja na taaluma ya benki na fedha,”alisema
Aidha, alisema mafunzo hayo ambayo yataendeshwa na maafisa waandamizi kutoka RSM Eastern Africa wenye uzoefu wa kimataifa yatasaidia ajenda ya maendeleo ya kimataifa.
Aidha, alisema mafunzo hayo yatasaidia kwenye kufikia lengo la nne la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa (UN Sustainable Goals) kuhusu elimu bora na hasa elimu ya ufundi na elimu ya fedha ambayo inatolewa na chuo cha CBE.
Alisema mafunzo hayo yatahitimishwa na mashindano a washiriki ambapo washindi watapewa nafasi za masomo kwa vitendo yaani internship na yatasaidia jitihada za chuo kuwaandaa wahitimu kwaajili ya soko la ajira.
Profesa Munishi alisema RSM imekuwa ikifanya kaguzi za hesabu za fedha CBE kwa miaka sita iliyopita na kwa miaka yote hiyo chuo kimekuwa ikipata hati safi na hoja ambazo wamekuwa wakiziibua CBE imekuwa ikizifanyia kazi.
“Mafunzo haya ni muhimu sana kwa wanafunzi wetu wa CBE na yatatolewa na watu waliobobea kwenye masuala ya ukaguzi hivyo naona wanafunzi mtakaoshiriki kwenye program hii mnabahati kubwa sana na yatasaidia ajenda ya maendeleo ya kimataifa,” alisema Profesa Munishi.
Alisema serikali imefanya maboresho makubwa kwenye mitaala ya elimu na moja ya eneo ambalo imesisitiza ni wanafunzi kusoma kwa vitendo na kwamba elimu ya fedha na biashara ipewe umuhimu wa kipekee.
“Kwa hiyo nyinyi wanafunzi ambao mnasomea uhasibu, fedha, benki na biashara mko katika mazingira mazuri ya kuajiriwa na kujiajiri mtakapomaliza masomo kwa sababu kila kitu duniani kwa sasa kinatoa umuhimu kwa fani hizo,” alisema
Naye Jovin Bhoke, ambaye ni Meneja wa Kodi wa Kampuni ya RSM, alisema kila mwaka huwa wanaadhimisha siku ya huduma kwa wateja kwa kufanya shughuli mbalimbali za kusaidia jamii.
Alisema katika shughuli hizo huwa wanaangalia ajenda za serikali na zile za kidunia ambapo kwa sasa wameangalia ajenda namba nne ya UN inayojihusisha na utoaji wa elimu bora.
“Tumechagua kuja CBE kwa sababu ni chuo kikongwe kwenye kutoa elimu ya biashara, kodi na elimu ya fedha na tutawashirikisha kile tunachokifanya ili wanafunzi wawe wanasoma kwa kwa vitendo masuala yanayohusu elimu ya fedha,” alisema Jovin
“Tutawaonyesha wanafunzi kwamba ni kweli kile wanachokisoma kwa nadharia kipo na kinafanyakazi katika ulimwengu wa kibiashara, tutawaonyesha ukaguzi unakuwaje na malengo yake ninini kwa hiyo watapata picha halisi kwamba wanachokisoma darasani kipo kwenye ulimwengu wa taaluma,” alisema
Alisema RSM ni taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya ukaguzi wa hesabu za fedha, elimu ya kodi, kutoa ushauri wa kitaalamu na ina uzoefu wa kimataifa wa kufanyakazi katika zaidi ya nchi 120 duniani katika mabara ya Afrika, Asia, Ulaya na Amerika
Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala Profesa Emmanuel Munishi, akizungumza na viongozi wa kampuni ya ukaguzi wa hrsabuya RSM kwenye semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wanafunzi wa CBE chuoni hapo jana Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE waliohudhuria mafunzo hayo hivi karibuni.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala Profesa Emmanuel Munishi, akizungumza kwenye semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wanafunzi wa CBE chuoni hivi karibuni
Meneja wa RSM akiendelea na mafunzo kwa wanafunzi wa CBE hivi karibuni jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...