Na Mwandishi wetu Zanzibar

Imeelezwa kwamba Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ambayo inatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali na International Fund for Agricultural Development – (IFAD) Tanzania Bara na Zanzibar itachangia katika kutekeleza mipango iliyopo ya kitaifa kwa kutumia rasilimali zilizopo hususan katika Uchumi wa Buluu ambapo huchangia kwa kiasi kikubwa katika kipato cha wananchi na hatimaye Taifa kunufaika kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Islam Mchenga Wakati akizungumza na Ujumbe wa IFAD pamoja na Timu ya Uratibu wa Programu ya AFDP Ofisini Kwake Mjini Unguja, Zanzibar.

“Tunaelewa kwa upande wa uvuvi wa bahari kuu, kuna ununuzi wa meli unaoendelea, tukiwa na meli zetu itaongeza tija kubwa kiuchumi na wananchi kuweza kujiajiri,” alieleza.

Tumefanya vizuri katika kilimo cha mwani; ni vizuri tunaweze kuona ni namna gani ya kuweza kubadilishana uzoefu na wenzetu wa Tanzania Bara, ili waweze kunufaika na hizo fursa zilizopo.
Ujumbe huo wa (IFAD) Umetembelea pia Ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi na utatembelea maeneo mengine yanayotekeleza Programu (AFDP) kisiwani Zanzibar na Unguja

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Dkt. Islam Mchenga akizungumza na Ujumbe wa IFAD uliomtembelea Ofisini Kwake Mjini Unguja Zanzibar.
 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Dkt. Islam Mchenga akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa shirika la IFAD uliomtembelea Ofisini Kwake Mjini Unguja Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...