Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Asasi ya Human Dignity and Environment Care Foundation(HUDEFO) Sarah Pima amesema wanaipongeza Serikali kwa jitihada inazochukua kuhakikisha matumizi mabaya ya plastiki yanakuwa hayapo.
Ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini waliohudhuria semina iliyoandaliwa na asasi hiyo yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusu athari zinazotokana na matumizi ya plastiki sambamba na utunzaji mazingira kwa ujumla.
HUDEFO imeandaa semina hiyo kwa waandishi kupitia mradi wake wa Extended Producer Responsibility(EPR)ambapo kwa mujibu wa Sarah Pima ni kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kufikisha ujumbe kwa jamii na wadau mbalimbali kuondoa matumizi mabaya ya taka za plastiki.
“Tunaipongeza Serikali yetu kwa jitihada inazochukua kuhakikisha matumizi mabaya ya plastiki yanakuwa hayapo sambamba na uwepo wa sheria na miongozo ambayo imewekwa kuhakikisha tunaendelea kuhifadhi mazingira na tunaendelea kupunguza plastiki.”
Kuhusu mradi wa EPR, amesema umekuja ili sasa waweze kushirikiana kama wadau mbalimbali katika hiyo nyanja au mnyororo mzima wa mifuko ya plastiki na kuwa na jukwaa la pamoja.
Pia kuhakikisha kanuni pamoja na sheria inakuja kwa ajili ya mzalishaji ambaye anazalisha plastiki aweze kuchukua hatua kwa ajili bidhaa yake anayozalisha mpaka mwisho inakuwa katika kuokoa mazingira
“Hivyo basi tunaamini kupitia kuwa na kanuni,miongozo pamoja na sheria itasaidia katika kuweka mazingira kuwa mazuri na tutakuwa katika mpango ambao ni sahihi kuhakikisha kuanzia ngazi ya chini ya mnyororo wa thamani wa plastiki kila mtu anafanya kazi yake na kila mtu anahusika
“Tunaamini wazalishaji ambao wamekuwa wazalishaji sana wa plastiki lakini kuna watu wanahusika na vifungashio wote wako katika biashara basi tusiendelee kupiga kelele tuje na suluhisho la kukaa mezani na wafanyabiashara, warejeleshaji,Serikali , watunga sera, ,waokota taka na wadau wote…
“Ili tuwe na suluhisho la pamoja na kuhakikisha mtu kwa nafasi yake anafanya kazi vizuri na hatimaye tutaendelea kuhifadhi na kutunza mazingira kwa pamoja.”
Akizungumzia waandishi wa habari , amesema wana nafasi kubwa katika kuhamasisha na kufikisha ujumbe kusaidiana na wadau mbalimbali.
“Sisi kama wadau wa mazingira tunatambua nafasi ya waandishi wa habari.Tunamani tuanze pamoja,twende pamoja na tuendelee pamoja tukiwa na waandishi wa habari katika kuhakikisha habari sahihi zinafika pande mbalimbali za Tanzania.
“Lakini pia tukishirikiana kuanzia mwanzo kuwajengea uwezo waaandishi wajue nini wanaandika , tusaidiane katika nyanja mbalimbali kuanzia upande wa serikali na wadau wote.”
Awali Mlezi wa waandishi wa habari ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TMF Dastani Kamanzi amesema msingi wa semina hiyo kwa waaandishi wa habari inalenga kuendelea kuwakumbusha na kuwajengea uwezo kuhusu tatizo la kimazingira.
“Tunaposema mazingira ni pamoja na kuzungumzia uchafuzi wa mazingira na hasa uchafu unaosababishwa na taka za plastiki. Kwa hiyo mafunzo haya ni muhimu kwasababu vyombo vya habari na waandishi wa habari wanalo jukumu la kuelimisha umma…
“Pia kuwawajibisha wenye mamlaka na wote ambao wanahusika kwenye hili suala la mazingira.Hivyo mafunzo haya yamehusisha waandishi wa habari kutoka maeneo mbalimbali nchini ili kuwa na uelewa suala zima la plastiki na madhara yake kwa jamii,”amesema.
Amesisitiza taka za plastiki zina madhara kwa afya,kimazingira na kwa binadamu lakini katika mustakabali wa
nchi yetu kwani huko mbele kama hizo plastiki zitaendelea bila
kudhibitiwa na wadau basi zitaharibu ikolojia na mazingira.
“Hivyo
waandishi wamefundishwa jinsi ya kufanya kazi yao kwa weledi ili
kuhakikisha umma unajua jinsi ya kudhibiti hizi taka ngumu.Tumeona
waandishi wanakosa uandishi wa habari za kina…
“Uandishi unalenga
kuwajibisha wenye mamlaka, kuwajibisha wadau wanaohusika na uchafuzi
unaofanyika na uzalishaji wa hizi plastiki,”amesema na kuwataka
waandishi waliopata mafunzo hayo kuyatumia vema kwa kuandika habazi
zinazogusa maslahi ya wananchi katika kukomesha taka za plastiki.
Home
HABARI
HUDEFO YAIPONGEZA SERIKALI MIKAKATI KUKOMESHA MATUMIZI MABAYA YA PLASTIKI, YATOA NENO KWA WADAU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...