Na Jane Edward, Arusha 

Waziri wa Mali asili na utalii Anjela Kairuki anatarajiwa kufungua tamasha la Wanawake festival litakalofanyika November 17 jijini Arusha .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa tamasha hilo Nengasu Werema amesema kuwa wameamua kuunga serikali mkono katika jitiada za kutangaza utalii ambapo Tamasha hilo linalenga kuwezesha kufikia idadi ya watalii milioni Tano ifikapo mwaka 2025.

Nengasu amesema katika kumtambua mwanamke katika sekta ya utalii,watafanya tamasha ambalo litashirikisha wanawake na wadau wa utalii kwa pamoja ili Wanawake waweze kushiriki kwenye sekta ya utalii.

“Tunataka kutangaza na kukuza sekta ya utalii kwani mada kubwa ya festival hii ni kuangalia namna ambavyo Wanawake wanaweza kujihusisha katika sekta ya utalii ambayo itawezesha kukua kwa uchumi wa Tanzania na wa mtu mmoja mmoja”alisema

Aidha katika tamasha hilo kunatajwa kuwa na tuzo mbali mbali ambazo zitatolewa kwa Wanawake vinara wa utalii lakini pia wataweza kutembekea vivutio vya utalii ikiwemo ya hifadhi ya taifa ngorongoro na na hifadhi ya tarangire.

Kwa upande wake afisa uhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa tarangire Jully Bede aliwapongeza Wanawake hao kwa kuandaa tamasha hilo na kuhaidi kuwapa ushirikiano ikiwemo kuwaeleza Wanawake fursa zilizopo kwenye hifadhi.

Naye mkurugenzi wa Wanawake na utalii Mercy Michael alisema  lengo la wao kuandaa tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake walioko kwenye sekta ya utalii ni kuhamasisha Wanawake kuunga mkono sekta ya utalii pamoja na kujifunza shughuli za utalii ambazo Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kuonyesha njia na fursa zilizopo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...