• Benki ya KCB ina matumaini makubwa ya ushindi kulingana na rekodi alizo nazo mpaka sasa.
Dereva wa mbio za magari, Karan Patel anayedhaminiwa na Benki ya KCB yupo tayari kukamilisha rekodi ili kuchukua ubingwa wa Michuano ya Mbio za Magari Afrika maarufu kama African Rally Championship yatakayofanyika mkoani Iringa-Tanzania wikiendi hii.
Dereva huyo na mshikaji wake Tauseef Khan kwa sasa wanaongoza ARC wakiwa wamesimama na pointi 120 jambo ambalo linawaweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji hilo endapo timu hiyo itafanya vyema katika raundi mbili za mwisho nchini Tanzania.
“Umekuwa mwaka wa mafanikio kwetu hadi sasa na tunatarajia kumaliza vema hapa Iringa (Tanzania) kwa kukusanya pointi za kutosha ili tuweze kutwaa ubingwa wa ARC. Lengo si kushinda tu bali ni kufanya kile kinachohitajika kukusanya pointi muhimu ili tushinde,” alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Ushirika wa Benki ya KCB Tanzania, Christine Manyenye alisema Benki hiyo kama wadhamini wa timu kuu ina matumaini makubwa ya kutwaa taji hilo kwa kuwa madereva hao wameonesha umahiri wa hali ya juu kwenye michuano iliyopita.
“Tunapojiandaa kwa mbio za Tanzania, ambazo pia zitahitimisha mashindano hayo kwa mwaka huu wa 2023, tuna imani na timu yetu ya KCB. Tangu awali, wamedhihirisha nia yao ya kutwaa ubingwa wa bara na wamebakiza raundi moja tu kutimiza ndoto hii,” alisema Manyenye.
Akiwa na kazi iliyoangaziwa na mafanikio ya ajabu, Karan ameonyesha mara kwa mara uwezo wake wa kusukuma mipaka ya kasi kwenye wimbo. Safari yake imefafanuliwa kwa saa nyingi za kufanya kazi kwa bidii na harakati zisizo na kikomo za bora zaidi."Kama benki, tunapenda kuwahakikishia azma ya kuendelea kuwekeza kwenye mchezo wa magari na michezo mingine.Tunaamini kwa kufanya hivi tunaboresha chapa yetu ya KCB na kuwa chapa bora Afrika,” alisema.
Raundi ya kwanza itafanyika Jumamosi eneo la Matembo Iringa na njia ya mwisho itafanyika Sao Hill Mafinga na kufanya jumla ya kilomita 370.Dereva huyo, na mwendeshaji wake Tauseef Khan kwa sasa wanaongoza msimamo wa ARC wakiwa na pointi 120, akifuatiwa kwa karibu na Jas Magat wa Uganda mwenye pointi 111.

Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa KCB Bank, Christine Manyenye akipeana mkono kumtakia Kheri mshiriki wa mbio za magari, Karan Patel ambaye amedhaminiwa na KCB Group kushiriki mashindano ya African Rally Championship yatakayomalizika jumapili mkoani Iringa. Kulia ni dereva mwenza, Tauseef Khan. Kilele cha mashindanon hayo makubwa Afrika yatafnyika Jumamosi na Jumapili katika Mkoa wa Iringa huku Karan Patel akipewa nafasi kubwa ya ushindi akiwa na alama 120 mpaka sasa.
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...