Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Ramadhan Bukini amezindua kampeni ya mkono kwa mkono ili kutangaza Fursa zinazopatikana Nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo huko Afisini kwake Karume House amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuanza Novemba 25 Mwaka huu na kurushwa moja kwa moja kupitia shirika hilo.

Alifahamisha kuwa kampeni hiyo itawashirikisha Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya zote za Zanzibar pamoja na Taasisi zinazohusika na uwezeshaji Wananchi ili kutoa fursa kwa taasisi hizo kuzitangaza fursa kwa jamii.

“ Kampeni hiyo inayolenga kuzitambulisha fursa zinazopatikana katika mikoa ya Zanzibar na mbinu za kuzifikia ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo.”alisema Mkurugenzi Bukini

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Zanzibar Juma Burhan Mohamed amesema kampeni hiyo itasaidia kutoa taarifa zinazohusu uwekezaji,fursa za kujiajiri pamoja na upatikanaji wa masoko jambo ambalo litasaidia kuwanyanyua wajasiriamali Nchini.

Kampeni ya mkono kwa mkono imeandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Wakala wa uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Taasisi ya Afisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa utendaji Serikalini (PDB) na Kampuni ya Mwananchi Communication ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi .
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Ramadhan Bukini akitoa ufafanuzi kuhusiana na kampeni ya mkono kwa mkono iliyoandaliwa kwa mashirikiano kati ya Shirika hilo,Maelezo Zanzibar ,Kampuni ya Mwananchi ,Taasisi ya Afisi ya Rais ufuatialiaji na usimamizi wa utendaji Serikalini (PDB), Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Wakala wa Uwezeshaji Wananachi kiuchumi (ZEEA) kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi, hafla iliyofanyika Karume House.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Asha Juma Khamis akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mkono kwa mkono kuelekea Mika 60 ya Mapinduzi,hafla iliyofanyika Karume House.

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uwezeshaji Wananachi kiuchumi (ZEEA) Juma Burhan Mohammed akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mkono Kwa mkono kuelekea Mika 60 ya Mapinduzi , hafla iliyofanyika Karume House.
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Mwananchi Communications Bakari Machumu akizungumza katika Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mkono Kwa mkono kuelekea Mika 60 ya Mapinduzi , hafla iliyofanyika Karume House.

Mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Muhammed Khamis akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mkono Kwa mkono kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi.

PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...