NA DENIS MLOWE,SUMBAWANGA


Zaidi ya wakazi 1000 wa mkoa wa Rukwa na maeneo jirani wamejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya Bure sambamba na uchangiaji wa damu kwa hiari utakaofanyika kwa siku mbili mjini hapa.


Katika zoezi hilo lililoandaliwa na redio Vos Fm Radio ya mjini Sumbawanga kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya mkoa Sumbawanga na kupima magonjwa mbalimbali yakiwemo ugonjwa wa kisukari homa ya ini uwiano kati ya uzito na urefu pamoja na shinikizo la damu.


Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Rukwa na maeneo jirani waliojitokeza katika zoezi hilo wamesema wamefurahishwa na huduma hiyo kutolewa Bure na imewasaidia kupunguza gharama za matibabu pindi wanapokutwa na magonjwa.


Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Sumbawanga Dkt Ismail Macha amesema upo umuhimu wa Kila mwananchi kuitambua afya yake kwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara na hivyo itamsaidia kuanza matibabu mapema.


Alisema zoezi Hilo la siku mbili limefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya watu kujitokeza kwa wingi Hali ambayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Radio Vos Fm ambayo imeonyesha ushirikiano mzuri na kubuni kitu ambacho ni kurudisha kwa jamii.


Mmoja wa waandaaji wa zoezi hilo la upimaji wa afya Bure na uchangiaji wa damu kwa hiari Dkt John Maulinge amesema zoezi hilo litakuwa ni endelevu na litawafikia wahitaji wengi zaidi.


Dkt Maulinge ameongeza kuwa lengo la zoezi hilo ni kuwakumbusha wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao ili kuwa na uelewe wa masuala ya afya na wasisubiri mpaka kutokee matamasha kama hayo ili kuepuka madhara yatokanayo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.


Amewataka wananchi kuacha mtindo mbovu wa maisha na badala yake kuzingatia ulaji mzuri kwa kuzingatia makundi yote ya vyakula na kufanya mazoezi.


Zoezi hilo la upimaji wa afya Bure na uchangiaji wa damu kwa hiari limepewa jina la AFYA FESTIVAL 2023 na kubeba kauli mbiu inayosena maisha ni
afya zawadi ya damu ni zawadi ya maisha.


Zoezi hilo la upimaji wa afya Bure sambamba na uchangiaji wa damu kwa hiari litadumu kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 17 na 18 mwezi wa 11 2023 ambapo pamoja na mambo mengine pia ushauri wa masuala mbalimbali unatolewa ikiwemo elimu ya afya.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...