· Katibu Mkuu akipongeza kwa ubinifu

Na Humphrey Shao,Michuzi TV

SERIKALI imevitaka vyuo vikuu kuwa na program atamizi na zile za uanagenzi ili kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kuhangaika kutafuta ajira wanapomaliza.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, wakati wa mahafali ya 58 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNICC.

Kwenye mahafali hayo kulikuwa na wahitimu 1,226 wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili (Masters Degree).

Alisema utandawazi umesababisha mabadiliko makubwa kwa kasi yanayogusa kila nyanja ya maisha hivyo ni muhimu kutafuta njia ya kukabiliana na mabadiliko hayo kwenye maisha.

Alisema wahitimu hao wanapaswa kutambua umuhimu wa elimu ya ujasiriamali waliyoipata chuoni hapo kwani itawafundisha namna ya kuwa wabunifu na kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.
“Kwa elimu mliyoipata mnatakiwa kwenda kutengeneza ajira kwa wengine badala ya kuwa tegemezi wa kuhangaika kutafuta kuajiriwa nyinyi nendeni mkajiajiri na kuajiri wengine,” alisema Dk. Hashil

“Nyinyi mmepata elimu bora kwa hiyo nendeni mkaitumie kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayosaidia ustawi wa jamii na chuo kimeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mnapotoka CBE mnakuwa na uwezo wa kujiajiri,” alisema

Aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa maono mazuri yaliyisababisha kuanzisha program atamizi ya baishara ambayo inawapa wanafunzi uwezo wa kujifunza usimamizi a biashara kwa vitendo wanapokuwa shule.

Alisema program hiyo na ile ya uanagenzi inawawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakiwa shule hivyo wanapomaliza masomo hawasumbuki kutafuta ajira.
Dk Hashil pia aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuanzisha masomo ya Shahada ya Uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA), mtandaoni kwani inaonyesha ujasiri na uthubutu wa CBE katika kutoa elimu bora na inayokidhi mahitaji ya sasa ya dunia.

“Kuzindua program hizi kunaweka iwango vipya vya ubora na upatikanaji wa elimu ya juu nawapongea kwa kufungua milango ya fursa kwa wanafunzi na wataalamu ambao wanatafuta kujiendeleza bila kujali umbali,” alisema

Alisema serikali ya awamu ya sita inathamini na kupongeza mafanikio ya chuo cha CBE na itaendelea kufanyia kazi changamoto ya miundombinu ya vyuo vyote vya elimu ya juu kikiwemo chuo hicho ili kuvuka changamoto hizo.

Alikitaka chuo hicho kuwaendeleza walimu wake na kuwekeza kwenye program za kisasa za kufundisha, mbinu za kujifunza na mitaala ili kuhakikisha elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.

“Wekezeni kwenye vifaa vya teknolojia madarasani ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia na chuo kifanye tafiti zinazolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kutoa rasilimali kwa walimu na wanafunzi kushiriki katika miradi ya utafiti na uvumbuzi,” alisema
Naye Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga,

alisema wahitimu hao wamehitimu katika masomo mbalimbali yakiwemo ya usimamizi wa biashara, masoko, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na ugavi.
Profesa Lwoga alisema chuo hicho kimejitahidi kwa kiwango kikubwa kuwafundisha wahitimu ili wanapohitimu waweze kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kuhangaika kutafuta ajira.

“Tangu mwaka 2022 tulianzisha program atamizi za biashara ambapo wanafunzi wetu wenye mawazo ya biashara na bunifu mbalimbali wanatuletea mawazo yao tunayalea na wanaweza kuanza kufanyabiashara wakiwa chuoni na tunashirikiana na taasisi mbalimbali,” alisema

“Kuna wanafunzi wa CBE wameanza kujiajiri wakiendelea na masomo na kwa sasa wamehitimu tunatarajia waendeleze biashara zao na wakaajiri wengine badala ya kusubiri kuajiriwa,” alisema.
 

 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, akimtunuku mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakati wa mahafali ya 58 ya chuo hicho ambayo yamefanyika Ijumaa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Sehemu ya wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakiwa kwenye mahafali hayo ya 58 ya chuo hicho katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.

 

Kaimu Mkuu a Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Lwoga, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa chuo hicho kwenye mahafali  ya 58 ya chuo hicho yaliyofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dk. Hashil Abdalah.
 

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, akizungumza katika Mahafali ya 58 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) ambayo yamefanyika Ijumaa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...