Na Fauzia Mussa, Melezo


Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar imepokea ndege ya Shirika la ndege la Discover Airline yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 280.

Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa ndege hiyo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Mkuu wa kitengo cha uhusiano Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar Mulhat Yussuf Said alisema hatua hiyo inapelekea ongezeko la Watalii na abiria wanaopokelewa Viwanjani hapo siku hadi siku.

Alifahamisha kuwa awali ndege hiyo ilijulikana kama Uero wings Discover na ilianza safari zake Zanzibar Juni 2021 ikifanya safari zake mara 2 kwa wiki na sasa ndege hiyo itafanya safari zake kwa wiki mara tatu ndani ya Zanzibar.


“hii ni hatua nzuri iliyofikiwa na Nchi yetu na pengine mwakani inaweza kuongeza safari zake,hivyo tunatarajia ongezeko kubwa sana la abiria hadi kuvuka malengo na kufikia abiria milioni mbili kwa mwaka kupitia ndege za kitalii zinazotua katika viwanja hivi.”alisema Mkuu huyo


Aidha alieleza kuwa ndege hiyo ni mara ya kwanza kuwasili Zanzibar toka kubadilishwa jina ikiwa imebeba abiria zaidi ya mia moja na kutarajiwa kuondoka na abiria zaidi ya mia moja na 50.


Aidha alifahamisha kuwa awali ndege hiyo ilipokuwa ikifanya safari zake ilikuwa na safari zake mara mbili kwa wiki na kwa sasa itakuwa inafanya safari zake mara tatu kwa wiki.

Hivyo, alisema hatua hiyo ni nzuri ambapo kwa mwakani itaweza kuongeza safari zake au kuongeza ndege nyengine kwa mujibu wa mazungumzo yao waliokubaliana.

Hivyo, alisema ujio wa ndege hiyo ni hatua nzuri kwa ongezeko la Uchumi wa Nchi na wanategemea kuvuka malengo.

Sambamba na hayo alifahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuboresha kiwanja cha ndege cha Pemba ili kuruhusu ndege kama hizo kutua katika kiwanja hicho.

Nao baadhi ya watendaji katika kiwanja hicho walisema ujio wa ndege za Kimataifa kunapelekea ongezeko la pato la Taifa na mtu mmojammoja. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...