Na. Damian Kunambi, Njombe.
Viongozi wa Chama Cha Mapinfuzi Mkoa wa Njombe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wamekabidhi kiasi cha sh. Mil 10.9 kwa famialia za ndugu saba waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea mnamo Octoba 13 mwaka huu katika kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoani Njombe na kuuwa watu hao saba na kujeruhi watu 18 ambao wote ni viongozi wa CCM ngazi ya Kata.
Akikabidhi fedha hizo kwa niaba ya Rais mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Deo Sanga ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali ngazi ya mkoa na wilaya ya Makete sambamba na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo amesema awali Rais Dkt. Samia alitoa pole lakini kwa mara nyingine tena ametoa pole kwa familia hizo za wafiwa pamoja na majeruhi.
" Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Tumekuja kuwashika mkono wa pole kwa niaba ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, anawapa pole sana wafiwa na pia anawaombea mlio majeruhi ambao bado mnaugulia majeraha mpone haraka ili muweze kuendelea na majukumu yenu ya kila siku" Amesena Sanga.
Aidha kwa upande wake katibu wa CCM Mkoani humo Julius Peter amesema lengo la fedha hizo ni kuwapa faraja walengwa na si kuwagombanisha familia hivyo amewataka walengwa hao wakafarijike badala ya kugeuza kuwa chanzo cha mgogoro na kuzigawa familia zao.
Thadei Tweve ni mmoja wa wafiwa hao amemshukuru Rais Dkt. Samia na kusema kuwa fesha hizo zitasaidia kulipia ada za watoto aliowaacha marehemu huku mmoja wa majeruhi hao Tumaini Sanga akimshuku Rais Dkt. Samia kwa msaada aliowapa.
Hata hivyo baada ya kuwatembelea wafiwa hao na majeruhi 16 amabo walisha ruhusiwa lakini pia viongozi hao wa CCM walifika katika Hospitali ya Consolata Ikonda ili kuwajulia hali majeruhi wawili ambao bado wanaendelea na matibabu hospitalini hapo ambapo kwa mujibu wa Matroni wa hospitali hiyo Angelina Mayao amesema kwa sasa hali za majeruhi hao zinaendelea vyema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...