Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Oparesheni wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Nassoro Sisiwaya jana Novemba 1,2023 ameongoza kampeni maalumu ya kukamata magari yanayotembe na taa moja jambo ambalo ni kinyume na taratibu za usalama barabarani.
Mbali ya kukamatwa kwa gari hizo pia amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali za mara kwa mara.
Kamishina Sisiwaya amesema hayo akiwa kwenye operesheni maalumu ya kukamata magari yanayovunja sheria za usalama barabarani nyakati za usiku.
Operesheni hiyo imeweza kukamata makosa 32 ambapo madereva wa magari 22 wamekamatwa kwa kosa la mwendokasi huku madereva saba wamekamatwa kwa kosa la kuzidisha abiria kati ya magari hayo saba magari mawili ni mabasi makubwa ya abiria wa mikoani huku magari matano ni aina ya coaster na magari matatu yameamatwa kwa kosa la ubovu.
Aidha zoezi hilo limefanikiwa kukamata magari 18 yenye taa moja maarufu kama chongo kati ya magari hayo 18 magari 15 yakiwa ni magari ya abiria huku 13 ni aina ya coaster na maroli matano.
Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani kinatoa onyo kali kwa madereva wote wanaoendesha vyombo vya moto hususani nyakati za usiku kuto kuingiza magari yao barabarani iwapo kina mapungufu ya aina yoyote.
Aidha Jeshi la Polisi Kikosi Cha usalama barabarani kinaendelea na operesheni hii ya kukamata madereva wa magari yanayovunja sheria za usalama barabarani kwa nchi nzima na tunaendelea kuchukua hatua kali ikiwemo kufungia leseni za madereva hao na kuwafikisha Mahakamani kwa watakao tiwa hatiani ,amesema.
.jpeg)

Baadhi ya magari yaliyokamatwa
Mkuu wa Oparesheni wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishina Msaidizi Nassoro Sisiwaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...