Na Pamela Mollel,Longido
Viongozi wa dini na mila mkoani Arusha,wamefanya sala maalum kumwombea Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa weka mazingira wezeshi kwa wachimbaji madini kufanya shughuli zao.
Kutokana na mazingira hayo kuwa mazuri na wezeshi umewasaidia wachimbaji wazawa akiwamo Bilionea Sendeu Laizer,kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.
Sendeu Laizer,akizungumza na wanachi zaidi ya elfu moja katika hafla hiyo,iliyofanyika katika Kijiji cha Mundarara,kilichopo wilayani Longido,alisema amani iliyoko Tanzania hasa wilayani humo imechangia wachimbaji kufanya shughuli zao kwa uhuru.
"Sisi wawekezaji katika Wilaya ya Longido tunafanya shughuli zetu bila kuwapo kwa usumbufu wa aina yoyote kutokana na mazingira rafiki yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kuvutia wawekezaji,"alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...