Kampuni ya ALAF LIMITED leo imetangaza rasmi udhamini wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wanaosoma MA Kiswahili katika chuo hicho kwa mara ya tano mfulululizo sasa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa wanafunzi hao, Meneja Masoko wa ALAF, Isamba Kasaka alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya hivyo kupitia ALAF Foundation kwa kuzingatia umuhimu wa lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

"Huu ni mwaka wetu wa tano mfulululizo Kwa ALAF kutoa udhamini kwa wanafunzi wa UDSM kama njia ya kukuza lugha ya Kiswahili," alisema.

Aliwataja wanufaika wa mwaka huu kuwa ni Issa Mwilima Makoye, Juditha Mwilolezi na Violeth Crebo Obimbo ambapo kila mmoja anapokea Tsh 2,935,000 za Kitanzania.

"UDSM mmetupa ushirikiano mkubwa katika zoezi hili la kuwadhamini wanafunzi na inatupa moyo wa kuendelea kuwadhamini wanafunzi kila mwaka" alisema Isamba.

Alisema ALAF imekuwa ikijihusisha na utoaji wa Tuzo za Fasihi ya Kiswahili kwa takribani miaka minne şaşa, tangu mwaka 2016, na daima Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamekuwa ni wadau muhimu sana katika mchakato wa utoaji wa tuzo hizo.

"Jambo hili pamoja na mambo mengine limelenga kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kuwa tunakitangaza Kiswahili ndani na nje ya nchi kwani lugha hii ni miongoni mwa tunu za taifa letu na urithi wa pekee tulioachiwa na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere" alisema Meneja huyo.

Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa UDSM, Prof. Pendo Malangwa aliishukuru ALAF Kwa jitihada zake za kukuza lugha ya Kiswahili na kuwataka wanafunzi hao watumie udhamini huu vizuri ili wawe Bora zaidi.

Alisema tangu kuanzishwa kwa ufadhili huo, tayari wanafunzi 15 wameshanufaika na baadhi yao wamefanikiwa kupata ajira sehemu mbalimbali ikiwemo UDSM.

Meneja Masoko wa ALAF Limited, Isamba Kasaka, akikabidhi hundi kwa Juditha Mwilolezi (kulia), mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) ikiwa ni udhamini wa Masomo ya Shahada ya Uzamili ya Kiswahili. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa UDSM, Prof. Pendo Malangwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Prof. Shani Mchepange.
 

Wanufaika wa ufadhili wa masomo ya Kiswahili ngazi ya Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na ALAF Limited wakati wa makabidhiano ya hundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...