Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil na Camel Cement zimekabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.

Mbali na kukabidhi hundi hiyo pia Kampuni ya Camel Oil imetoa misaada mbalimbali kama Magodoro, maji na mablanketi kwa ajili ya waathirika hao na hiyo ni sehemu ya kampuni kurejesha tabasamu kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo yaliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya milioni 100 pamoja na mahitaji hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha na msaada huo vifaa hivyo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.

"Tumepokea Sh.milioni 100 kutoka Camel Cement lakini na vitu vingine kutoka Camel Oil na tunaomba kwa niaba ya Serikali mtupelekee salamu kwa menejiment tunashukuru.

"Bado tunahitaji misaada ya kibinadamu ili kuwezesha ufumbuzi wa muda na wa kudumu kwa ajili ya ndugu zetu ili maisha yarejee kama kawaida " amesema Waziri Jenista.

Awali wakati abakabidhi misaada hiyo Meneja Masoko na Uhusiano wa Umma wa Amsons Group, Bhoke Rioba amesema Camel Cement imeweka fedha kwenye akaunti ya maafa ya Serikali kiasi cha Sh.milioni 100, magodoro 100 pamoja na mashuka 100.

Amesema kutoa kwao fedha na msaada huo ni muendelezo wa kampuni hizo kwenye kampeni yake ya kurudisha tabasamu kwa jamii ya Tanzania.
Meneja Uhusianoo wa Umma wa Amsons Gruop Bhoke Rioba(kulia) akikabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama (wa pili kushoto)kwa ajili ya mfuko wa maafa kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dk.Mollel


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...