Na Mwandishi

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imetoa wataalam sita wa saikolojia na masuala ya ustawi wa jamii ambao wameungana na wataalamu wengine kutoa huduma katika kambi tatu za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe Hanang mkoani Manyara.

Akipokea wataalam hao, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, amesema kutokana na maafa yaliyowapata waathirika hao ambao wamepoteza ndugu na mali zao na  kupata msongo wa mawazo na hivyo wanahitaji kujengwa kisaikolojia kwa kuwapa matumani ili kuendelea kuishi na kurejea katika hali yao ya awali.

Pamoja na hilo Katibu Mkuu Yonaz amempongeza Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo kwa hatua hiyo kwa kusema timu ya DCEA itaungana na wataalam wengine waliopo kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia wananchi  kwa kuwapa huduma ya unasihi (ushauri) pamoja na elimu ya kujikinga na magonjwa ya afya ya akili wanapoendelea kuhudumiwa na Serikali.

“DCEA imetoa Wasaikolojia hawa ambao watajikita kutoa elimu kwa waathirika wa maafa yaliyotokea, hii ni hatua nzuri kwa kuwafikia na kuwashauri pale inapobidi ili kusaidia kutopata msongo wa mawazo na kupambana na changamoto ya afya ya akili,” amesema Dkt. Yonazi

Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka Daniel Kasokola, amesema Kamishna Jenerali wa Mamlaka amechukua hatua ya kutuma timu hiyo kama sehemu ya kutekeleza mwito wa Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwataka watanzania wote kuungana kuwataidia wahanga hao na anaamini kuwa,  timu hiyo kwa kushirikiana na wataalam nyingine itaaidia waathirika wa maafa hayo ili warejee katika hali zao za kawaida.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...