Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu akikabidhi tuzo katika kongamano la 14 la mwaka la kongamano la wataalam wa ununuzi na ugavi, lililofanyika leo tareh 12//2023 katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC Jijini Arusha
Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu akihutubia katika kongamano la 14 la mwaka la kongamano la wataalam wa ununuzi na ugavi, lililofanyika leo tarehe 12//2023 katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC Jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wa kongamano la 14 la mwaka la kongamano la wataalam wa ununuzi na ugavi, wakisikiliza Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu wakati wa ufunguzi katika kituo cha kimataifa cha mikutanoAICC jijini Arusha leo tarehe 12/12/2023
Na.Vero Ignatus,Arusha
Taarifa ya utendaji ya PSPTB imesema kuwa ipo changamoto kubwa ya baadhi ya wataalamu waliobainika kufanya kazi pasipokuwa na sifa stahiki na bila kusajiliwa na bodi kama ilivyo takwa la kisheria kifungu cha sheria cha PSPTB,kwani inachangiwa na waajiri kuruhusu kazi za ununuzi kufanywa na waajiriwa nje ya taaluma ya ununuzi na ugavi ambayo kwa ukubwa wake imeinazigusa ofisi YA Rais Tamisemi yenye watumishi wengi zaidi wa kada hiyo
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusna na Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba katika kongamano la la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi,ambapo amemuelekeza katibu mkuu wa wizara ya fedha kushirikiana na Bodi kukutana na Katibu Mkuu Tamisemi ,Katibu mkuu Utumishi wa Umma kwa utatuzi wa changamoto hiyo ili kuhakikisha kazi za ununuzi na ugavi zinafanywa na wataalam wenye sifa nz waliosajiliwa na bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ya PSPTB
Dkt Mwigulu amesema pamoja na kutambua juhudi za PSPTB katika kusimamia taaluma ya ununuzi na ugavi amepokea changamoto ya maslahi madogo kwa wataalam haswa wanaohitimu cheti cha kitaalam cha CPSP ukilinganisha na taaluma zingine kama uhasibu na sheria
“Serikali inatambua kuwa ununuzi unachukua sehemu kubwa ya bajeti ya serikali na hivyo mchango wawataalam hawa lazima utahaminiwe ili wataalam waweze kufanya kazi bila vishawishi”alisema Dkt.Mwigulu .
Kupitia hotuba yako na taarifa ya utendaji wa majukumu ya Bodi ya Wataalam wa
Ununuzi na Ugavi (PSPTB) nimesikia kuwa mfumo wa usajili wa wataalam wa
ununuzi na ugavi kwa njia ya mtandao unasomana na Mfumo wa Taifa wa
ununuzi (NeST) ili kuhakikisha shughuli za ununuzi na ugavi zinafanywa na
wataalam wenye sifa stahiki waliosajiliwa na PSPTB.
Hatua hii itasaidia kwenye udhibiti wa weledi wa wataalam kuhakikisha wataalam wanaotumia mfumo huu ni wenye sifa za kitaaluma na waliosajiliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi naUgavi.
Nitumie fursa hii kuwaelekeza waajiri wa Sekta zote kuhakikisha wataalam
wanaofanya shughuli za ununuzi na ugavi wana sifa sitahiki za kufanya kazi hizo
kama ilivyoainishwa kwenye Sheria Na. 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha Bodi ya
Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), pamoja na miongozo inayotolewa.
Akinukuu kutoka kwenye taarifa ya utendaji Dkt.Mwigulu amesema kuwa pamoja na changamoto ya maslahi imeeelezwa kuwa PSPTB imekuwa na changamoto ya utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kisheria ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa wataalam wake nchini nzima,katika sekta umma,binafsi ,kuwajengea uwezo wataalam na wadau kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi na kufanya utafiti wa kitaalam ili kuleta ufumbuzi wa usimamizi bora wa mnororo wa ununuzi na ugavi kwasababu ya ufinyi wa bajeti
Hivyo amemuagiza Katibu Mkuu wizara ya Fedha kuangalia uwezekano wa kuisaidia PSPTB Kupata fedha kufanikisha majukumu hayo,Vilevile Dkt.Mwigulu amewataka psptb kuwapatia watanzania kazi ili waweze kuwaajiri wageni siyo kila mara wageni ndiyo wanawaajiri wazawa kwa kutumiataaluma na ujuzi wao kasha wanaandika ripoti kwa kutumia utendajikazi wa Watanzania
“Kazi hizi ni zakufanya kizalendo wapeni watanzania kazi,kasha wao wawape wagenikazi jamani,wekeni upendeleo kwa wenye nchi yao,nchi tajiri zote duniani uchumi wake unashikiliwa na sekta binafsi “alisema.
Nimefurahi kusikia kuwa, PSPTB chini ya usimamizi wa Bodi yako imeendelea
kusimamia maadili na mienendo ya Wataalam kwa kuchukua hatua za kinidhamu
kwa wataalam wanaokiuka miiko ya taaluma yao, niwapongeze sana kwa hatua
hii. Hivi karibuni nimeshuhudia mkichukua hatua kwa Wataalam walionekana
kutekeleza majukumu yao chini ya kiwango cha taaluma yao kupitia taarifa ya
ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (GAG) na Mamlaka
ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA). Niwatake kuendelea kuchukua hatua zaidi
ili kuilinda taaluma hii muhimu.
Aidha itakumbukwa kuwa katika hotuba ya wizara ya fedha iliyosomwabugeni ya mwaka 2023/2024 ilitoa dira ya hotuba ya serikali kuhakikisha ununuzi unafanyika kwa njia ya mtandao kwa kuzingatia bei halisi ya soko ili kupunguza gharama katika ununuzi wa umma na kuleta tija kw aTaifa katika utekelezai wa mnyorororo wa ununuzi wa ugavi nchini
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PSPTB Jacob Jail Kibona katika kongamano hilo ametaja baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana tangia kuundwa kwa bodi kwa sheria ya bunge namba 23 ya mwaka 2007 ,amesema bodi hiyo imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha psptb kwa kusimamia kukuza fani ya ununuzi na ugavi nchini,ambapoimeendelea kuuhisha mitaala ya mafunzo ya kitaalam na kuzalisha wataalam wenye ujuzi na umahili.
Aidha PSPTB imeendelea kudhibiti ubora wa taaluma kwa kupitia mitaala ya vyuo na taasisi nyingine zaelimu ya juu zinazotoa mafunzo ya fani ya ununuzi na ugavi nchini sambamba na kuendesha mitihani ya kitaaluma kwa watahiniwa katika fani ya stashahada ya kitaalam na stashahada ya kitaalam ya cheti cha kitaaluma cha juu kwa wanaofanya kazi ya ununuzi na ugavi
Kongamano hilo la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi limebeba mada isemayo mabadiliko ya kidijitali katika kuboresha usimamizi wa mnyororo wa ununuzi na ugavi kwamaendeleo endelevu .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...