Picha ya pamoja ya Jukwaa la Anthpolojia mara baada ya kukutana jijini Dar es Salaam.
Mwanajukwaa la Anthpolojia Dkt.Richard Sambaiga akitoa maelezo kuhusiana na kazi ya jukwaa hilo katika jamii ,jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
CHAMA cha Anthpolojia kimesema kuwa matatizo mengi yanatokea pasipo kuangalia kiini katika jamii husika kilichosababisha hivyo chama hicho kinakwenda kuwa suluhisho.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt.Vendelin Simon ambaye Mhadhiri Idara ya Socialojia na Anthplojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa kuanzishwa Jukwa hilo litasaidia kufanya tafiti na kutoa majibu katika jamii.

Amesema nchi nyingi zimeweza kuwa na majukwaa ya Anthpolojia na kuwa sehemu ya msaada katika nchi zao ambapo Tanzania ndio jukwaa limeanzishwa kwenda kusaidia jamii inayotuzunguka.

Aidha amesema kuwa katika kutekeleza majukumu ya jukwaa hilo ni kwenda kufanya tafiti kwa vyanzo mbalimbali vya fedha na kuweza kuishauri Serikali namna ya kuchukua hatua.

Amesema watalaam wapo ambao wanatakiwa kuwa kila sehemu zinazotoa huduma kwa jamii katika kushughulika na matatizo kwa uchambuzi wa kiini hicho ndipo kazi ya kada hiyo inakwenda kuonekana.

"Tumedhamiria kuanzisha jukwaa hili sio kwa ajili ya kutambua kada ya Anthpolojia bali ni kwenda kushughulika na matatizo ya jamii yetu na kuleta matokeo chanya".amesema Dkt.Simon

Dkt.Simon amesema kuwa Anthpolojia inajumuisha kada mbalimbali ambao wanakwenda kushughulika na jamii moja ndio maendeleo.

Nae Mhadhiri wa Idara ya Socialojia na Anthpolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Richard Sambaiga amesema kuwa watalaam wa Anthpolojia kulikuwa hakuna jukwaa la kuunganisha lakini sasa ndio tumefikia kuanzisha katika kwenda kuhudumia watanzania katika nyanja mbalmbali.

Kwa upande wa Mtafiti Mkuu wa NIMR Elizabeth Shayo amesema Anthpolojia iko katika uwanja mpana hata katika afya wanahitahitajika kufanya tatifi katika milipuko mbalimbali katika jamii kabla ya kutoa suluhisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...