NA FARIDA MANGUBE - MOROGORO

Matumizi mabaya ya Madaraka ukaidi kwenye usimamizi wa sheria, unaofanywa na asilimia kubwa ya viongozi wa serikali za vijiji, kwenye usimamizi wa Rasilimali ardhi ndio kiini cha migogoro ya kila mara kumekwisha ripotiwa mauaji, Uharibifu wa mali ikiwemo Mifugo na mazao ya kilimo, baadhi ya watu kusalia na ulemavu wa kudumu hayo yote yakisababishwa na mwingiliano wa shughuli za kibinadamu.


Mkoa wa Morogoro ni kati ya meneo ambayo kwa miaka mingi kumekua na migogoro, baina ya watumiaji wa ardhi ambayo husababishwa na mwilingiliano wa shughuli za kibinadamu, kwenye matumizi ya ardhi ikijumuisha Kilimo, ufugaji na Uhifadhi hasa katika wilaya za Kilombero, Malinyi, Kilosa na Mvomero maeneo yenye idadi kubwa ya watu wanaovitiwa na uwepo wa maeneo makubwa ya ardhi yenye Rutuba, ardhi oevu na mabonde makubwa.

Kijiji cha Utengule katika Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro miongoni mwa vijiji vya pembezoni mwa hifadhi ya Pori la akiba la Kilombero lililopandishwa hadhi kutoka pori tengefu la Kilombero kupitia tangazo la Serikali namba 64 la Februari 17 mwaka 2023.


Ndani ya Pori la akiba Kilombero kuna idadi kubwa ya watu walioanzisha makazi ya kudumu wakiendesha pia shughuli nyingine za kibinadamu ikiwemo Kilimo, ufugaji na Uvuvi hali ambayo imesababisha kuwepo mgogoro baina yao na mamalaka inayosimamia Pori hilo.

Justina Kulwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Utengule amesema alianza kuishi na kufanya shughuli za Kilimo ndani ya eneo la Pori la akiba Kilombero mwaka 2016 baada ya kukalibishwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ambaye jina lake limehifadhiwa, aliambiwa wazi eneo hilo ni sehemu ya hifadhi lakini aendelee na shughuli zake ikiwemo kuishi na familia yake kwakua Serikali ya kijiji hicho imepanga kubadilisha matumizi kuwa eneo la Kilimo na makazi.

“Niliuziwa Heka kumi ndani ya eneo la Pori la akiba la Kilombero kwa shiringi Milioni Mbili na laki nane Tsh.2,800,000 na mtu ambae sikuwa namfahamu kwa kipindi hicho na mauziano yalifanyika mbele ya viongozi wa vijiji na tumeandikishiana siwezi kusema moja kwa moja kama kinacho tuponza ni hawa viongozi hawajui sheria ya umiliki wa ardhi ninacho kiona ni taamaa zao zinafanya kushindwa kutuambia ukweli”. Alisema Ramadhani Minza miongoni mwao wenye makazi eneo la hifadhi.

Sheria ya ardhi namba tano ya mwaka 1999, imetoa wajibu wa usimamizi wa ardhi ya vijiji kwa Halmashauri ya Kijiji ikisisitiza utekelezaji wake kuzingatia haki na wajibu wa taasisi na mamlaka nyingine hata hivyo Halmashauri ya Kijiji inafanyakazi kama mdhamini kwa niaba ya wanufaika ambao ni wanakijiji kwa maana hiyo chombo chenye madaraka ya mwisho katika usimamizi wa ardhi ya kijiji ni Mkutano Mkuu wa kijiji.


Ugawaji wote wa ardhi ya kijiji lazima uthibitishwe na Mkutano Mkuu wa Kijiji, Suala ambalo halifanyiki katika maeneo mengi ikishuhudiwa mauziano yanayofanyika kinyemela baina ya mnunuzi na baadhi yao viongozi.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa katika moja ya hotuba zake aliposema “Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne kuchangia maendeleo vitu hivyo ni Ardhi, Siasa safi, Uongozi Bora na Watu”.Huenda Mwalimu alimaanisha ardhi ni miongoni mwa misingi Madhubuti ya maendeleo ambayo endapo viongozi wakiongozwa na siasa safi, kutakuwa na utumiaji mzuri wa ardhi hiyo kwa ajili ya yetu na vizazi vijavyo.


Mwaka 2019 Serikali kupitia Wizara ya ardhi nyumba na makazi iliamuru watumishi wote wa sekte ya ardhi katika Mkoa wa Morogoro kuhamishwa vituo vyao vya kazi na kwenda maeeo ya mikoa mingine lakini hata baada ya utekelezaji huo bado imeshuhudiwa kuwepo migogoro ya ardhi , ikionesha kiini ni kukosekana kwa usimamizi wa sheria.


Kwa Tanzania upatikanaji wa ardhi huwezeshwa kwa njia kadhaa ambazo ni halali na zinazokubalika kisheria katika jamii ikiwemo kutwaa hii hutumika pale ambapo mtu huingia katika pori na kulisafisha kisha kuliweka kwenye matumizi linaweza kuwa ardhi ya kijiji au hifadhi, kurithi, kugawiwa na Serikali, kununua pamoja na upangishaji,

Justina Kulwa akiwa kwenye makazi yake ndani ya Pori la akiba Kilombero akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii, nyuma yake ni eneo la shamba lenye mazao mbalimbali yakiwemo mahindi pamoja na kibanda cha jiko analotumia kupikia kwenye eneo hilo la makazi yake lenye nyumba tatu.
PICHA 3. Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Utengule walio na makazi ya kudumu na kuendesha shughuli za kibianaadamu ikiwemo kilimo na ufugaji ndani ya Pori la akiba Kilombero wakifuatilia kwa karibu mkutano uliotishwa na kamati ya ulinzi na usalma Wilaya ya Kilombero kwa lengo la kuwata kutoka ndani ya pori hilo.
Pichani ni mashamba na makazi ya kudumu yaliyo anzishwa ndani ya eneo la hifadhi ya Pori la Akiba Kilombero.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...