Na.Khadija Seif,Michuziblog
SERIKALI ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imesema ina mpango wa kuboresha masoko yake makuu ikiwemo soko la Temeke Sterio, Tandika na Keko yaweze kufanana kama soko kuu la Kariakoo.
akizungumza Leo Disemba 19,2023 katika Maeneo tofauti tofauti ya Wafanyabiashara wa soko la Temeke Sterio, Tandika na Keko kwenye ziara yake kwenye wilaya ya Temeke, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Janeth Masaburi amesema masoko hayo yakikarabatiwa yataweza kuwa kivutio na ongezeko la wateja kutoka ndani na nje ya nchi kuja kununia bidhaa kwenye soko hilo.
"Haya masoko natumaini yatakuwa ni masoko ya mfano kwa sababu yatakwenda kuleta wateja wengi Sana, kwa hiyo nawaomba viongoozi wa masoko mlisimamie hili"alisema Janeeth.
Pia mbunge Janeth amewakumbusha wafanyabiashara wa masoko hayo kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao wanayofanyia biashara ili kisudi maeneo yao yao yawe kivutio kwa watu wanaofika kutembelea masoko hayo kwa kununua bidhaa pamoja na wafanabiashara wenyewe kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Mbunge Janeth Masaburi pia ametoa majiko ya gesi na mkaa mbadala kwa mama lishe na baba lishe wanaofanya biashara ya kuuza chakula kwenye masoko hayo ili kisudi waweze kuachana na matumizi ya kupikia kuni na mkaa ambayo yanaharibu Mazingira na kusababisha kutopata mvua za kutosha.
Naye Meneja wa Masoko ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa masoko yaliyopo kwenye wilaya ya Temeke Godfrey Asukile amefafanua zaidi kwa ukarabati wa masoko hayo matatu Temeke Sterio, Tandika na Keko unatarajiwa kufanyika mwanzoni 2024 na unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 600.
Aidha amesema masoko hapo pia yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mapaa machajavu ya soko, mitaro , kizimba cha taka na uongezaji wa matundu ya vyoo pamoja na miundombinu ya soko kwa ujumla.
Mbunge Janeth anafanya muendelezo ya ziara yake ambapo Disemba 6 mwaka huu, kwa kufanya ziara kwenye kata ya Pugu, Jimbo la Kibamba na Ubungo, Jimbo la Kawe wilaya ya Kinondoni na Jimbo la Temeke wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Janeth Masaburi akizungumza na Wafanyabiashara wa soko la Temeke Sterio na kuwakumbusha kufanya usafi wa Masoko hayo kabla ya kusubiri Manispaa kufanya ukarabati wa jumla wa Masoko hayo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Janeth Masaburi akiwaunga mkono Wafanyabiashara wa Soko la Tandika mara baada ya kufanya ziara katika Masoko ya Wilaya ya Temeke Leo Disemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam
Mama Lishe katika soko la Temeke Sterio akikabidhiwa mtungi wa gesi na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Janeth Masaburi mara baada ya kutembelea sehemu hiyo ya chakula wanachopika Mama lishe zaidi ya 10 ndani ya soko la Temeke Sterio Jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...