Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba ili kuendelea kuwepo rasilimali ya maji ardhini hapa Zanzibar ni lazima kuchukuwa hatua na kutilia maanani suala la uhifadhi wa Mazingira, kupanda miti na kutunza uoto wa asili ulipo usipotee.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko Masingini wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja alipofungua mradi wa Uimarishaji na Uhuishaji wa Mfumo wa Usamabazaji maji Zanzibar, ikiwa ni shamra shamra za sherehe za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Mhe. Othman amefahamisha kwamba kufanya hivyo ndio kuieneleza rasilimali hiyo iendelee kuwepo na kuwanufaisha wazanzibari na kwamba utunzaji wa mazingira ndio unaozalisha maji.

Amesema kwamba ni jukumu la kila mwananchi na viongozi katika ngazi mbali mbali kuutunza mradi huo kimazingira na kimiundombinu ili kuhakikisha kwamba mradi huo ni wa watu wote na kwafaida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Amefahamisha kwamba ulezi wa wa miradi ya aina hiyo ni ya watu wote na kwamba kila mmoja anawajibu wa kushirikiana kuulea ili uweze kuwa endelevu na kuwa na manufaa Zaidi kwa wananchi.

Mhe. Othman amesema kaatika kutilia mkazo suala utunnzaji wa Masingira serikali kupitia Ofisi yake itazindua mradi mkubwa wa upandaji miti katika visiwa vyote vya unguja na Pemba jambo litakalohitaji ushiriki wa kila mwananchi na viongozi ili kuufanikisha kurejesha Zanzibar kuwa ya kijani.

Mhe. Mhe. Makamu amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanalipa bili za maji kwa kuwa kufanya hivyo ndio kuiufanya miradi ya maji kuwa endelevu na kuendelea kuwanufaisha wananchi wa Zanzibar.

Aidha amesema kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelipa umuhimu mkubwa suala la maji kwa kufanya juhudi za kuhakikisha ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya aina mbali mbali mbali ya maji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Joseph John Kilangi amewatahadharisha wananchi wanaoliongiwa na watakaoungiwa majini na mita kuhakmikisha kwamba hawazichezei ili kuziharibu.

Amesema kwamba jumla ya wananchi milioni moja na laki tano wataunganishwa kwenye mfumo wa kisasa wa smati mita na kuwataka wananchi wote kuendelea kuitunza miundo mbinu sambamba na kuwa na subra wakati serikali ikiendelea na mipango ya kukamilisha malipo ya vipando kwa wananchi waliopitiwa na mradi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA Dk . Salha Mohammed Kassim amesema kwamba mradi huo umegharimu dola za Marekani milioni 92.18 na utekelezaji wa mradi umenza Aprili mwaka 2020 ambao umegaiwika katika sehemu tatu za utekelezaji.

Aidha amesema kwamba skimu ya Masingini imejumuisha uchimbaji wa visima vinane vikubwa ambavyo vimekamilika na vinauwezo wa kuzalisha lita lakini nane na tiisi alfu kwa saa ambao utawanufaisha wananchi wa shehia ya Masingini , Mtufaani,Mwera na Mwembe mchomeke ambapo kazi ya ulazaji wa mabomba imekamilika.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo cha Habari

Leo tarehe 27.12.2023

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman ,Masoud Othman , akizungunza katika ufunguzi wa Mradi wa Maji Masingini wakati Mhe. Makamu alipofika Masingini magharib A Unguja kuzindua rasmi mradi huo leo tarehe 27.12.2023. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kushoto) , akipokea zawadi kwa Meneja wa Mradi wa Maji Masingini kutoka Kampuni ya L&T ya nchin India wakati Mhe. Makamu alipofika Masingini kuzindua maradi huo leo tarehe 27.12.2023. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman ,Masoud Othman , akifungua pazia kuashiria ufungunzi rasmi wa Mradi wa Maji Masingini wakati Mhe. Makamu alipofika Masingini magharib A Unguja kuzindua rasmi mradi huo leo tarehe 27.12.2023. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...