Na Janeth Raphael - Michuzitv Dodoma.
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lakamilisha Mchakato wa kuandaa Andiko Dhana linaloainisha umuhimu wa Sekta ya Ujenzi kulingana na jukumu waliopewa la kuratibu uandaaji wa Sheria ya majengo Nchini.
Hayo yameelezwa na Geofrey Ibrahim Mwakasenga ambaye ni Mhandisi Ujenzi katika Baraza la Taifa la Ujenzi katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika Leo hii Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa Hadi Sasa.
"Kulingana na jukumu ambalo Baraza lilipewa la kuratibu uandaaji wa Sheria ya majengo Nchini,tunapenda kuwajulisha hatua iliyofikiwa Hadi Sasa. Kwa Kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali na za Binafsi, Baraza la Taifa la Ujenzi limekamilisha mchakato wa kuandaa Andiko Dhana linaloainisha umuhimu wa Sekta ya Ujenzi,pamoja na changamoto zinazojitokeza kwasasa, Andiko hilo kwasasa lipo Wizarani Ujenzi kwaajili ya hatua nyingine".
Aidha Mhandisi Mwakasenga ameeleza kuwa Ujenzi wa Majengo kwasasa unasimamiwa na Sheria nyingi kwa kukosekana Sheria moja maalumu ambayo husababisha usumbufu katika uendelezaji wa majengo na gharama zisizo za lazima kwa waendelezaji wa majengo.
"Kwasasa Ujenzi wa majengo unasimamiwa na Sheria nyingi mbalimbali, kwasababu ya kukosekana Sheria moja maalumu, hivyo kusababisha usumbufu katika uendelezaji wa majengo na gharama zisizo za lazima kwa waendelezaji wa majengo.
Kutokana na hilo Serikali kupitia Wizara ya ujenzi iliamua uandaliwe mfumo Bora wa kisheria wenye kanuni na miongozo inayojitosheleza utakaotumika katika Usimamizi wa Ujenzi wa majengo Nchini".
Pamoja na hayo amesema kuwa uwepo wa Sheria ya majengo Nchini utawezesha kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa Usimamizi wa Ujenzi wa majengo wenye uwezo wa kudhibiti uharibifu wa mazingira,ubora,usalama na Afya.
"Pamoja na faida nyingi zilizopo, uwepo wa Sheria ya majengo Nchini utawezesha kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa Usimamizi wa Ujenzi wa majengo wenye uwezo wa kudhibiti uharibudu wa mazingira, ubora, usalama na Afya".
Kwa upande wake Afisa Habari wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Bwana Elieza Rweikiza ameongeza kuwa anaamini Sheria ya majengo itakuwa imeboreshwa na kuwekwa vitu ambavyo havipo katika Sheria zilizopo.
"Tunapoongelea Sheria ya majengo tunamaanisha kwamba itakuwa imeboreshwa ili vitu vingine ambavyo havipo kwenye Sheria zilizokuwepo viweze kuingizwa mule ndani".
"Na kuongeza: kwamba ziko taasisi zinazosimamia Wahandisi, Wakandarasi na watu wote wanaoshughulika katika Sekta ya Ujenzi,lakini Sheria inapokuja maana yake mapungufu yaliyopo kule yanawekwa pamoja ili yaweze kuwasilishwa kwa pamoja na hilo jukumu litakuwa linasimamiwa na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi".
Moja Kati ya majukumu ya kisheria yanayosimamiwa na Baraza hili ni pamoja na kuhamasisha na kuweka mikakati ya kukuza,kuendeleza na kupanua Sekta ya Ujenzi Nchini Tanzania hususan kwa kujenga uwezo wa ushindani wa wazawa ili waweze kushindana na kutekeleza miradi kwa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Pia kuratibu na kuwezesha utatuzi wa migogoro inayotokea katika miradi ya Ujenzi kwa ufanisi.
Mhandisi Ujenzi katika Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Geofrey Mwakasenga (kulia),akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 21,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea masuala muhimu kuhusu sheria ya majengo nchini ambapo NCC inaratibu uandaaji wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...