Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuendelea kufanya utafiti wenye lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii ya Zanzibar na kutoa ushauri wa kitalaamu.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika Mahafali ya Kumi na Tisa (19) ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) ukumbi wa Dkt.Mohamed Ali Shein Kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja tarehe: 28 Disemba 2023.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimejiandaa kuhakikisha vijana wote wenye sifa za kujiunga na Vyuo vikuu wanapatiwa mikopo ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza wahitimu Wanawake kwa kushika nafasi za juu na kufikia asilimia hamsini na nane (58) kati ya wahitimu 2,102 wa Chuo hicho.

Pia katika mahafali hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima katika fani ya Usimamizi wa Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...