Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuendeleza Sekta ya kilimo kwenye mazao ya chakula na Biashara.

Amesema lengo ni kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa chakula na kila Mtanzania anayejishughulisha na kilimo aweze kukuza kipato chake na uchumi Taifa kwa ujumla.

Amesema hayo leo Disemba 29,2023 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Juhudi B kwenye kata ya Chinongwe, Ruangwa mkoani Lindi.

Amesema Rais Dkt. Samia wakati wote amedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa kimbilio la wengine wanaohitaji mazao “Tumuunge mkono Rais wetu kwenye mapambano yake ya kukuza sekta ya kilimo, amefanya makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kuagiza kutengwa kwa maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana”
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...