NA FARIDA MANGUBE MOROGORO

Vaileth Kawovela mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Kibaha mkoani Pwani, mwanamke asiyejutia kuzaliwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, alijitambua kuwa katika hali hiyo akiwa na miaka 12 na kutumia vema Dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV) na sasa amefanikiwa kuwa na mtoto wake wa kwanza aliyethibitishwa na wataalam kuwa hana maambukizi.

Safari ya Maisha kwa Vaileth haikuwa ngumu, alipewa taarifa kuwa ameathirika mapema tangu akiwa mdogo na mama yake mdogo baada ya wazazi wake kufariki, tangu hapo hakuona sababu ya kujutia hali aliyokuwa nayo jambo ambalo limemsaidia kufanya maamuzi ya kuanza kutumia Dawa na sasa imethibitishwa na Madaktari amefanikiwa kufubaza virusi mwilini mwake na hawezi kuambukiza mtu mwingine.

“Nimejifungua kwa njia ya kawaida, Madaktari walimfanyia uchunguzi wa awali mwanangu pia kunipatia Dawa za kumkinga ambazo nilikuwa nampatia kila siku ambapo walipomfanyia uchunguzi wa mwisho wamebaini hana mambukizi lakini bado naendelea kumlinda mtoto wangu”. Alisema.Vaileth Kawovela mkazi wa Kibaha mkoni Pwani mwanamke asiyejutia kuzaliwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI akiwa na mtoo wake siku chache baada ya kujifungua .

Yeye na mwenza wake wote wanaishi na maambukizi ya VVU walikutana kwenye kambi za vijana wanaoishi na Virusi vya UKIMWI chini ya Mradi wa CDC/PEPFAR afya ni hatua unaotekelezwa na shirika la Tanzania Heath Promotion Support (THPS) ambapo walianzisha mahusiano na kufikia kupata mtoto wao huyo wa kwanza wa kiume, mpango wao ni kufunga ndoa kuendelea kuishi pamoja mwaka 2024.

Amehimiza jamii hasa wanawake waliofikia Umri wa kuzaa kujijengea utamaduni wa kupima afya mara kwa mara, kujiandaa aidha kwa kuwakinga watoto wao dhidi ya maambukizi ya magonjwa ikiwemo UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto jambo rahisi endapo mzazi atajitambua mapema.


“Kwa mujibu wa wataalamu wa afya nimefikia kiwango ambacho virusi haviwezi kuonekana kwenye mashine hii inamaanisha siwezi tena kumuambukiza mtu mwingine, hata kwa mtoto wangu imekuwa rahisi kumlinda na maambukizi tangu akiwa tumboni na hata wakati wa kujifungua na hii ni matokeo ya kuzingatia matumizi sahihi ya Dawa za ARV”. Aliongeza Vaileth.Pichani Vaileth Kawovela kipindi cha ujauzito wake

Wanatambua malengo ya kidunia kufikia mwaka 2023 ni asilimia 95 watu wote Ulimwengunu kuwa wanatambua hali zao kwa kupima VVU, asilimia 95 ya waliotambua hali zao na kubainika wanaishi na maambukizi wawe wanatumia Dawa na asilimia 95 ya wanaotumia Dawa kuwa wamefubaza Virusi kenye miili yao kiasi cha kutoweza kumuambukiza mtu mwingine hivyo kuondoa uwezekano wa kuwepo maambukizi mapya.


Evodius Gozbelt ambae ndie mwenzawake na Vaileth nae ni mwenye furaha muda wote anasema sasa yeye na mwenza wake wameelekeza nguvu kumtunza mtoto wao kwa kufuata maelekezo ya wataalam, ingawa tayari vipimo maalum kuonesha wingi wa virusi mwilini Target Not Directed (TND) kimeonesha wawili hao wamefanikiwa kufubaza kabisa Virusi mwilini kiasi cha kutoweza kumuambukiza mtu mwingine.

Msisitizo wao jamii kuongeza umakini kwenye kuzingatia malezi na makuzi ya watoto wao, wakisema pamoja na kuwa wawili hao wanaishi kwa furaha ingewezekana pia wasingekuwa katika hali hiyo kuzaliwa wakiwa na maambuziki endapo wazazi wao wangetilia maanani suala la kufuatilia afya zao, hii ni moja ya sababu ya kujiweka wazi kutaka kufikishia jamii elimu ya malezi kwa watoto.Pichani ni Evodius Gozbelt akiwa na mwenza wake Vaileth Kawovela wenye nyuso za furahi Likiwa ni ishara ya kutojutia kuishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI
“Nakumbuka kipindi nipo mtoto jinsi ambavyo tulikuwa tunahudumiwa tukifika Kliniki tunacheza nao kama watoto wezetu, wanatusukuma kwenye bembea, tulikuwa tunapewa chama na vimaziwa Fulani, ilikuwa inatupa furaha kwa kuwa tuliwa tunakutana na watoto wengine ilitufanya kupenda kutumia dawa za ARV bila hata kujua, hivyo ni meva watoa huduma wakaendeleza utaratibu huu kuondoa hali ya unyanyapaa na usiri inapobidi kwenye maeneo ya huduma”. Alisema Gozbelt.


Kwa mujibu wa wataalam wa afya Mama mjamzito mwenye maambukizi ya VVU anapaswa kuhudhilia Kliniki kama wajawazito wengine, na kufuatilia kwa karibu maelekezo ya Daktari pamoja na kutumia dawa za ARV, ufuatiliaji huo hufanyika kipindi chote cha ujauzito pia wakati na baada ya kujifungua kuepusha uwezekano wa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Matokeo ya awali ya utafiti wa viashiria na matokeo ya UKIMWI nchini Tanzania wa mwaka 2022-2023 uliosimamiwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia tume ya taifa ya kuthibiti UKIMWI tacaids umeonesha makadirio ya takribani watu 1,500,000 wenye umri wa kuanzia miaka 15 wanaishi na maambukizi ya VVU, huku takribani watu 60,000 kwa kila mwaka hupata maambukizi mapya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...