Na Muhidin Amri,Tunduru
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali kukuza na kuboresha sekta ya
elimu hapa nchini,Chama kikuu cha ushirika wilaya ya
Tunduru(Tamcu)kimetoa msaada wa mifuko 20 ya saruji na mchanga lori
mbili kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule ya kulea watoto
ya Hannover Day Care.
Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Biblia Tanzania,inajihusisha kutoa
elimu na malezi kwa watoto wadogo wilayani Tunduru,inakabiliwa na
changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo na ukumbi kwa
ajili ya kulia chakula.
Akikabidhi msaada huo kwa mwalimu mlezi na mwenyekiti wa bodi ya shule
hiyo,Meneja mkuu wa Tamcu Iman Kalembo amesemaTamcu imeamua kutoa msaada
huo ili usaidie katika ujenzi wa vyoo na madarasa li kuwawezesha watoto
wapate sehemu sahihi ya kujifunzia na kujistili.
Kalembo alisema,huo ni mwanzo katika kuhakikisha shule hiyo inakuwa na
mazingira bora na rafiki ya kufundishia na kujifunzia na kuwa kimbilio
la wazazi wanaotafuta sehemu sahihi kwa ajili ya elimu ya watoto wao na
jamii ya wana Tunduru ambao kwa muda mrefu wamebaki nyuma kielimu.
Ametoa wito kwa wadau wengine wakiwemo wazazi wenye watoto wanaolelewa
katika kituo hicho kushirikiana na uongozi wa kituo hicho ili kujenga
mazingira rafiki ambayo yatawasaidia watoto kukua katika malezi mazuri
na kuimarika kitaaluma.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Mchungaji Emmanuel Telela
alisema,msaada huo umewafungulia njia kuanza maandalizi ya kufyatua
tofali kwa ajili ya kuongeza vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo na
kuboresha miundombinu ya shule hiyo.
Amewaomba, wadau mbalimbali wenye moyo na wanaoguswa na changamoto hiyo
kujitokeza ili kuwasaidia watoto wanaolelewa katika shule hiyo ili
waweze kuboresha mazingira ya shule kwa kuongeza idadi ya madarasa na
matundu ya vyoo.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Martha Chowo alisema,saruji
waliyopata itasaidia kuongeza idadi ya madarasa na kufanya ukarabati wa
vyoo vinavyotumiwa na watoto.
Alisema,katika shule hiyo wanachukua wanafunzi wenye umri kuanzia miaka
miwili hadi mitano na kwa sasa wamebaki watoto 13 baada yaw engine 16
kumaliza elimu ya awali miezi miwili iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...